26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

CHINA YAISIFU TANZANIA KWA SERA YA UWAZI

Na Ismail Ngayonga-MAELEZO


 

CRJESERIKALI ya China imeisifu Tanzania kwa kuzingatia sera ya uwazi katika ushindanishaji wa zabuni za miradi ya ujenzi, ikilinganishwa na nchi nyingine zilizopo katika ukanda wa  Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki.

Hayo yamesemwa hivi karibuni mjini hapa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CRJE ya nchini China, Hu Bo wakati  akizungumza na waandishi wa habari  wa Kituo cha Televisheni ya Taifa ya nchi hiyo (CCTV) waliofika nchini kujionea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali yao nchini Tanzania.

Mwenyekiti huyo alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zinazoongoza kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu za zabuni za ujenzi, ambapo Serikali ya Tanzania imekuwa ikitoa kipaumbele kwa makampuni ya ukandarasi ya wazawa kwakukubali maombi yao ya zabuni za ujenzi.

“CRJE inafanya shughuli zake katika mataifa mbalimbali ya Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda, katika sehemu zote hizoTanzania imekuwa  nchi bora zaidi kwani pamoja na mazingira bora ya kazi zetu lakini pia wakandarasi wazawa wamekuwa wakipewa nafasi katika miradi ya ujenzi,” alisema Hu Bo.

Kwa mujibu wa Hu Bo tangu mwaka 1977 kampuni hiyo imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi nchini Tanzania, hatua inatokana na ushirikiano na uhusiano wa kirafiki uliopo baina ya Serikali ya China na Tanzania.

Alitaja baadhi ya  miradi ya Serikali iliyokamilishwa  kampuni hiyo nchini ni pamoja na ujenzi wa ukumbi wa Bunge Dodoma, Jengo  la Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Jengo la Ofisi ya Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar, Ofisi za Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles