NA Joseph Lino,
Kampuni ya Mihan Gas Limited ambayo inajihusisha na uagizaji na usambazaji wa jumla na rejareja wa nishati ya gesi ya LPG, wiki hii inakuelezea chimbuko nzima la Mihan Gas ilikotoka hadi kufikia nyumbani.
Gesi ya Mihan inajulikana kama Liquefied Petroleum Gas (LPG) inatokana na malighafi ya mafuta mazito (Crude Oil) ambayo ni tafauti na gesi ya asilia ambayo inajulikana kama Liquefied Natural Gas (LNG).
Lakini leo tunazungumzia chimbuko la gesi ya LPG ambayo kwa sasa ndio inatumika kwa wingi katika matumizi ya kupikia nyumbani na viwandani.
Kabla kutengenezwa kuwa gesi ya LPG, nishati ya mafuta hupatikana ardhini ikiwa ni mchanganyiko wa uozo wa viumbe na mimea iliokufa kujisindika kwa miaka mamilioni yaliyopita.
Uozo huu unazalisha nishati ya mafuta kadhaa ikiwemo petroli, diseli, mafuta ya ndege, mafuta ya taa pamoja na gesi ya nyumbani (LPG) ambayo inasambazwa na kampuni ya Mihan.
Gesi ya LPG kwa matumizi ya nyumbani
Gesi hii ni kwa jili ya matumizi ya nyumbani ndio mana kampuni ya Mihan iliona uhitaji wa Watanzania hasa gharama kubwa wanazotumia katika kupika chakula kutumia mkaa, mafuta taa, kuni na umeme.
Baada ya kuona tatizo hilo walifikiria kuja bidhaa ya Mihan Gas ambayo inamlenga kila Mtanzania kuanzia wa kipato cha chini hadi juu.
Meneja wa Masoko na Mauzo wa Mihan Gas, Veneranda Masoum anasema gesi ya LPG hutoa moto na joto la uhakika hivyo kufanya mapishi kuwa rahisi, haraka, kufurahisha na safi.
“Mihan Gas haiachi madoa au masizi kwenye vyombo vya kupikia, haichafui chakula na husaidia kupunguza muda wa kupika pamoja kuimarisha vyombo vya kupikia,” anasema.
Ujio wa Mihan Gas katika soko la Tanzania kama nishati ya kupikia itaweza kusaidia kupunguza athari mbaya ya afya kwa Watanzania ambao sasa hutumia majiko ya mkaa, mafuta ya taa au kuni ambayo kutoa moshi au hewa yenye madhara carbon monoxide.
LPG ni gesi ya kupikia kwa kuanzia watu wa hali chinihadi wale wa juu na hivyo nchi nyingi zilizoendelea zinatumia hiyo kwa kupikia kwani ni bora na safi na vilevile muafaka.
Ili kufanya uchaguzi wa nishati gani utumie wakati wakupikia inaenda sanjari na sababu kadhaa zenye faida.
Ushawishi wa uamuzi wako unatokana na urahisi wa upatikanaji, unafuu na matumizi rahisi na usalama.
Gesi ya Mihan iliyotengenezwa mahususi kwa kila Mtanzania itaweza kusaidia mtu yoyote kuanzia wa kipato cha chini hasa kipindi hiki ambacho kuna mdororo wa uchumi duniani.
Mihan gesi ni sulisho kwa Watanzania ambao wanataka kuendelea kuwa na maisha bora kipindi hiki cha upatikanaji thamani halisi ya fedha zako (Value for money). Ina vigezo vyote ambavyo watu wanavitafuta.