23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mwijage achagiza kuwekeza kwenye viwanda

 WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage

Na Mwandishi Wetu,

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, amewataka Watanzania kuwekeza kwenye viwanda na kuachana na dhana potofu ya kufikiria kuwa viwanda lazima viwe vikubwa na kutumia mtaji mkubwa.

Aliwataka kuona uwekezaji wa viwanda kama shughuli mojawapo ya kuzalisha mali kisheria ambapo watu wanaajiriwa kufanya kazi na bidhaa zake kutumika sokoni kama imefikia kiwango husika.

“Unapokuwa na kiwanda unazalisha kitu au mali mpya na hivyo kukuza utajiri wa nchi,” alisema.

Waziri Mwijage aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Sensa ya mwaka 2013, ikiwa ni ya nne kuhusu Hali ya Uzalishaji Viwandani Tanzania Bara iliyofanyika Dar es Salaam hivi karibuni.

Vilevile Mwijage amezitaka mamlaka mbalimbali za nchi kuwezesha viwanda vidogo vidogo  vya wajasiriamali ili virahisishe mipango ya kufanya nchi iwe na uchumi wa viwanda kwa kasi zaidi.

Mwijage aliliagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kutekeleza azimio la kupunguza bei ya umeme kwa wajasiriamali kwa viwanda vidogo ambavyo huajiri vijana wengi. Kwenye bei mpya zinazoombwa na Tanesco kwa EWURA suala hilo limezingatiwa.

Sensa ya mwaka 2013 ya Uzalishaji Viwandani Tanzania Bara ni ripoti iliyofanywa kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Chama cha Wenye Viwanda (CTI) na Shirika la  Umoja wa Mataifa Maendeleo ya Viwanda  (Unido) na hivyo ni taarifa rasmi za hali ya viwanda, ingawa ni muda mrefu toka itolewe mwaka wa mwisho.

Mwijage anasema takwimu zinaonesha kufikia mwaka 2013, Tanzania ilikuwa na viwanda 49,243 huku asilimia 99.15 kati ya hivyo, ni viwanda vidogo na vidogo zaidi.

Kisera viwanda vimeainishwa katika  mafungu manne ikizingatiwa idadi ya wafanyakazi wake, ambapo vile viwanda vidogo zaidi vinaajiri mtu mmoja hadi wanne na vile vidogo ni kati ya watu 5 na 49  na vile vya kati ni watu 50 na 99 na viwanda vikubwa vina wafanyakazi zaidi ya  100 na kuendelea.

NBS imesema Sensa hiyo ni ya nne baada ya miaka 24 na nyingine ni zile za 1963, 1978, na 1989. Ukweli wenyewe ni kuwa ni Viwanda vyenyewe ndivyo vinachagua mwaka wa Sensa.

Suala la kuwa nchi ya uchumi wa viwanda ndio msingi na mhimili wa nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles