24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Chid Benz: Dawa za kulevya kwangu itabaki historia

Rashidi Makwiro ‘Chid Benz’
Rashidi Makwiro ‘Chid Benz’

NA ESTHER GEORGE,

RAPA mkali katika muziki wa Bongo Fleva, Rashidi Makwiro ‘Chid Benz’, amesema matumizi ya dawa za kulevya yamempa mafunzo makubwa na itabaki kuwa historia kwake.

Chid Benz aliliambia MTANZANIA kwamba dawa za kulevya zimeharibu maisha yake kwa kiasi kikubwa na yamemdhalilisha yeye na familia yake na watu wake wa karibu hivyo hatathubutu kurudia kama baadhi ya wasanii walioacha na kurudia kama Rehema Chalamila ‘Ray C’.

“Dawa za kulevya kwangu zinabaki kuwa historia, sitaki hata kuzisikia zimeniumiza sana kimawazo, zimenidhalilisha na zimepoteza mwelekeo wa maisha yangu, sina hamu nazo tena nina hasira nazo siwezi kuzirudia kama baadhi ya wengine walivyorudia kwa sasa naangalia maisha yangu mapya katika muziki,” alijieleza Chid Benz.

Chid Benz anaeleza kwamba waliomshawishi kuingia katika matumizi ya dawa hizo ni marafiki zake katika makundi aliyokuwa akibadilishana nao mawazo ambao wengi wao walimshawishi kwamba akitumia dawa hizo atakuwa na nguvu zaidi ya kuimba na kufanya makubwa jukwaani lakini ikawa tofauti na matarajio.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles