27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Chemical: Young D alinitia hasira

chemical1NA THERESIA GASPER

MSANII wa miondoko ya hip pop, Claudia Lubao ‘Chemical’, amefunguka kuwa aliingia kwenye fani hii mara baada ya kumuona msanii, Young D akifanya vizuri kwenye tasnia hiyo.

Alisema msanii huyo alikuwa na umri mdogo lakini mashairi yake yalikuwa na akili nyingi kiasi kwamba alikuwa kivutio kwa wengi jambo ambalo lilimhamasisha naye akaingia katika muziki huo kwa kasi.

“Mimi na Young D tupo sawa kiumri, nikaona hata mimi naweza kufanya kama yeye anavyofanya ndiyo maana nikaamua kuingia kwenye tasnia hii ili niweze kuwaonyesha Watanzania kwamba hata wasichana tunaweza hip pop kama wavulana wanavyoweza,” alieleza.

Msanii huyo ana lengo la kuitangaza zaidi hip hop kimataifa kama wakali mbalimbali wa muziki huo wanavyofanya akiwemo Joh Makini ambaye ndiye msanii anayemvutia katika muziki huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles