27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Chelsea kuvaana na Manchester City FA

chelseaLONDON, ENGLAND

RATIBA ya mzunguko wa tano wa michuano ya Kombe la FA imewekwa wazi, ambapo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini England, Chelsea, wanatarajia kukutana na Manchester City kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Huu ni mchezo ambao unatarajiwa kugusa hisia za mashabiki wa soka kutokana na uwezo wa klabu hizo na kuwa na mashabiki wengi duniani.

Kocha wa Chelsea, Guus Hiddink, amesema kuwa huo utakuwa ni mchezo ambao utawakusanya mashabiki wengi kama ilivyo katika michezo ya fainali.

“Naweza kusema kuwa huu utakuwa ni mchezo wa fainali kwetu, timu zote zina wachezaji wenye uwezo mkubwa, hivyo natarajia kuona mashabiki wengi katika mchezo huo,” alisema Hiddink.

Wakati huo klabu ya Ligi Daraja la Kwanza, Shrewsbury Town, ambayo imeonesha ushindani wa hali ya juu, itakuwa kwenye Uwanja wa New Meadow dhidi ya wapinzani wao, Manchester United.

Mabingwa watetezi wa michuano hiyo ya Kombe la FA, Arsenal, watakumbana na Hull City, ambao walikutana katika fainali mwaka 2014. Hii itakuwa ni mara ya tatu mfululizo klabu hizi kukutana katika michuano hii, huku mwaka jana, Arsenal ikiishambulia klabu hiyo kwa mabao 2-0.

Michezo mingine ambayo itapigwa ni pamoja na Reading dhidi ya West Brom au Peterborough, Watford dhidi ya Leeds, Blackburn dhidi ya Liverpool au West Ham, wakati huo Tottenham ikipambana na Crystal Palace, huku Bournemouth ikicheza na Everton.

Michuano hiyo inatarajia kuendelea kutimua vumbi Februari 19, mwaka huu, kwenye viwanja mbalimbali.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles