28.2 C
Dar es Salaam
Monday, February 6, 2023

Contact us: [email protected]

Ronaldo ampagawisha Zinedine Zidane

RonaldoMADRID, HISPANIA

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amempagawisha kocha wake, Zinedine Zidane, baada ya mchezaji huyo kufunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Espanyol.

Mchezaji huyo amekuwa akitajwa kwamba kiwango chake kimeshuka kwa kiasi fulani, lakini Zidane amesisitiza kwamba bado mchezaji huyo yupo katika ubora wake kutokana na ushindi huo.

Mabao hayo yamemfanya awe sawa na mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez, mwenye mabao 19, sawa na mchezaji huyo.

“Ronaldo ana mchango mkubwa sana katika klabu hii, kila mtu anajua hilo, kama angefunga mabao chini ya matatu lingekuwa ni jambo la kawaida, lakini kwa kuwa amefunga mabao matatu basi sifa yake inazidi.

“Ninaamini ushirikiano wa Ronaldo na Karim Benzema utaifanya klabu hii kuleta mapinduzi makubwa msimu huu,” alisema Zidane.

Hata hivyo, klabu hiyo hadi sasa inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi ikiwa na alama 47, huku Barcelona ikiwa na alama 51, wakiongoza ligi hiyo wakifuatiwa na Atletico Madrid wenye alama 48.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles