26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Chelsea inaweza kufanya maajabu kwa PSG leo?

544LONDON, ENGLAND

LIGI ya Mabingwa barani Ulaya, inatarajia kuendelea leo kwenye viwanja viwili ambapo ni Stamford Bridge jijini London na Petrovsky uliopo nchini Urusi.

Kwa upande wa jiji la London, leo litasimama kwa muda kuupisha mchezo kati ya wenyeji Chelsea ambao watawakaribisha wapinzani wao, PSG kutoka jijini Paris nchini Ufaransa.

Hapa lazima mbabe apatikane ambaye ataingia hatua ya robo fainali katika michuano hiyo. Mchezo wa awali PSG ilikuwa nyumbani na ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, hivyo katika mchezo wa leo inahitaji ushindi wa aina yoyote ili kuweza kusonga mbele au sare.

Wakati huo Chelsea wanatakiwa kushinda bila ya kuwaruhusu wapinzani wao kupata bao, hapo watakuwa wamepata nafasi ya kusonga mbele.

Mchezo huo unaonekana kuwa mgumu kwa kuwa kila klabu ina wachezaji wenye uwezo na kila mmoja anataka kuipigania timu yake kusonga mbele, hivyo chochote kinaweza kutokea.

Mchezo mwingine ambao utapigwa kule nchini Urusi ni kati ya wenyeji Zenit dhidi ya Benfica ya nchini Ureno.

Katika mchezo wa awali Benfica walikuwa nyumbani na walifanikiwa kushinda bao 1-0, ni wazi kwamba ushindi huu ni mwembamba na wanaweza wakawa na wakati mgumu ugenini japokuwa wanahitaji ushindi au sare ya aina yoyote kuweza kusonga mbele.

Lakini wenyeji lengo lao kubwa ni kushinda ushindi wa mabao zaidi ya moja na inawezekana kwa kuwa wapo nyumbani na wanaweza kuutumia uwanja wao vizuri mbele ya mashabiki wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles