24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Cheki mastaa wa Marekani walivyopiga pesa!

jay-z

Na MARKUS MPANGALA

MUZIKI ni kazi ambayo imeajiri mamilioni ya watu kote duniani. Ingawa sina takwimu sahihi lakini wanamuziki wengi sana wamekuwa wakipata fursa za kutumbuiza kwenye matamasha au hekaheka za uchaguzi kwenye nchi mbalimbali.

Uchaguzi Mkuu wa kisiasa katika mataifa mengi wanamuziki au wasanii wamekuwa chachu ya ushindi wa baadhi ya viongozi tulionao leo hii.

Uchaguzi wa Marekani umefanyika Novemba 8 mwaka huu. Kuna wanamuziki wengi waliojitokeza kuwaunga mkono wanasiasa wawili waliogombea kiti cha urais, Hillary Clinton wa Chama cha Democrat na Donald Trump wa Chama cha Republican.

Kwa upande wao Democrat kilipata uungwaji mkono na huduma za wanamuziki Madonna, Jay Z ‘Jigga’ na Beyonce. Tunafahamu kuwa Jay Z ni miongoni mwa majina makubwa duniani yenye sifa kubwa kwenye muziki.

Yeye alianzisha lebo yake ya Rocafella mwanzoni mwa miaka 2000, kabla ya kuibadili na kuuita Roc Naton. Ameshiriki matamasha mbalimbali. Ni mwanaumuziki aliyetajirishwa na sanaa hiyo kiasi cha kuitwa bilionea.

Beyonce naye ni mwanamuziki aliyeanzia Kundi la Destiny Child enzi hizo akiwa na Michelle pamoja na Kelly Rowland. Hawa waliunda kundi hilo wakiwa na vipaji vikali, kabla ya baadaye kufanya kazi binafsi.

Wimbo wao wa Survivor ulitingisha sana na kuwapa heshima kubwa, binafsi nilikuwa shabiki wa kundi hilo. Ushirikiano wa kimuziki kati ya Jay Z na Beyonce umeleta ndoa ambayo sasa wana mtoto mmoja. Wimbo wao wa Crazy in Love ni kitu kingine kinachowaacha kwenye ramani ya muziki.

Wanamuziki hawa wote walimuunga mkono Hillary Clinton kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Jay Z, Beyonce na Madonna wana ushawishi mkubwa katika jamii.

Uamuzi wao wa kumuunga mkono Hillary hauwezi kuja bure hivihivi bila malipo ya kazi zao. Jay Z na Beyonce walitumbuiza katika kampeni za Hillary ikiwa na maana dau la kuwapata na mapenzi yao vilikuwa vitu muhimu vilivyozingatiwa na timu ya kampeni ya Hillary.

Wasanii wengine waliomuunga mkono Hillary ni Rapa Big Sean, Queen Bey, Sigourney Weaver, Lee Daniels Taraji P. Henson, Bryshere Gray, Trai Byers, Jussie Smollett, Tasha Smith, Gabourey Sidibe na Grace Byers.

Kwa upande wa Donald Trump waliomsapoti ni Jon Voight, Scott Baio, Ted Nugent, Kid Rock, Mike Tyson kwa kutaja wachache.

Tofauti ya wasanii hawa ni moja; kwa upande wa Hillary walikuwepo kwenye majukwaa na walitumbuiza. Kutumia kazi zao za jukwaani maana yake Democrat walilipia huduma hizo za burudani na si vinginevyo.

Kwanini nimekumbusha jambo hilo? Mwaka 2015 tulishuhudia wimbi kubwa la wasanii wakishiriki kampeni mbalimbali za wagombea wa uchaguzi.

Katika uchaguzi huo kulikuwa na kambi mbili; Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyompigia kampeni Dk. John Magufuli na wengine walijiunga na kambi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyoungana na vyama vingine kuunda Ukawa.

Naandika kuwapa somo wasanii wetu nchini. Wakati wa kufanya kazi kwa mapenzi umekwisha. Uchaguzi wa wowote unapofanyika nchini ni lazima wauchukulie kuwa suala la kazi siyo burudani.

Kwa kawaida burudani inayotolewa ni kazi iliyolipiwa. Nafahamu pia vyama vya CCM na Chadema vililipia burudani za wasanii hao.

Hata hivyo kumekuwa na wimbi la hofu la kuwaudhi washabiki wao. Wasanii wa namna hiyo wanatakiwa kujiuliza kuwa kazi yao ni kutumbuiza bure au biashara?

Kwenye Uchaguzi Mkuu kunakuwa na malefu ya watu wanaohitaji burudani. Chama kinapoomba ridhaa ya wananchi maana yake kinatafuta pesa.

Na mwanamuziki au msanii anatafuta pesa. Ni mwiko kwa mwanamuziki kuruhusu kazi yake itumike bure huku baada ya muda mfupi anaanza kulia njaa.

Wasanii wetu wachukulie masuala ya uchaguzi kama sehemu ya kazi ambayo inawaingizia pesa na si mahaba eti unakipenda chama fulani. Hivyo vyama vikishapata wanachokitaka kwa msanii havina mpango nao tena mpaka uchaguzi mwingine.

Naamini kutumbuiza kwa Jay Z na Beyonce kwenye kampeni za Hillary kulilipiwa fedha nyingi ambazo hazijawaacha patupu.

Wasanii wetu wanatakiwa kufahamu kuwa wanapotumbuiza wakati wa kampeni ni shughuli rasmi ambayo inatakiwa kulipiwa ili kuondokana na malalamiko kutioshwa baada ya uchaguzi.

Ni jambo ambalo linatakiwa kuwa wazi, katika kazi hakuna mapenzi  na urafiki, inakubidi usimamie kazi kwanza, mapenzi ya kuvipenda vyama yawe baadaye tena ya zaidi ya mno.

Usisahau kuwa tayari Rais Mteule wa Marekani ni Donald Trump.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles