23.6 C
Dar es Salaam
Thursday, May 9, 2024

Contact us: [email protected]

Chapecoense kupewa ubingwa wa Copa Sudamericana

3ad814ee00000578-0-image-a-1_1480410133341

MEDELLÍN, COLOMBIA

KLABU ya Atletico Nacional ambayo ilitarajia kucheza mchezo wa fainali ya Copa Sundamericana na klabu ya Chapecoence ya nchini Brazil, imekitaka Chama cha Soka America ya Kusini (Conmebol) kutoa ubingwa kwa wapinzani wao.

Kauli hiyo imetolewa jana kutokana na wachezaji wa klabu hiyo ya nchini Brazil kupata ajali ya ndege na kupoteza maisha mwanzoni mwa wiki hii.

Chapecoence ambayo ilikuwa inashiriki Ligi Kuu nchini Brazil mara baada ya kupanda daraja mwaka 2014, ilitarajia kushuka dimbani jana dhidi ya wenyeji Atletico Nacional ya nchini Colombia katika fainali ya Copa Sundamericana.

Ajali ya ndege hiyo ambayo ilitokea usiku wa manane, inadaiwa kusababishwa na matatizo ya umeme.

Ndege hiyo ilibeba watu 81 wakiwemo abiria 72 na ndani ya abiria hao walikuwapo wachezaji na viongozi wa timu hiyo, ambapo hadi sasa inadaiwa wachezaji wawili wapo hai kati ya msafara mzima, huku watu 77 wakipoteza maisha.

Kutokana na hali hiyo, klabu ya Atletico Nacional imewaomba viongozi wa kombe hilo la Conmebol kutoa ubingwa kwa klabu hiyo ambayo imepoteza maisha ya wachezaji.

Kupitia mtandao wa klabu hiyo ya Atletico Nacional, wamedai hakuna sababu ya wao kuchukua ubingwa huo wakati huo wapinzani wao wamepoteza maisha, ni bora kombe hilo wakapewa wao kwa ajili ya kukumbukwa.

“Tunajua kila mmoja ameguswa na tukio hilo, hakuna aliyefurahia kusikia kwamba wapinzani wetu wamepata ajali na kupoteza maisha.

“Ajali hiyo ni sawa wameipata kaka zetu wa Chapecoense, jambo ambalo haliwezi kufutika kwa kila mmoja wetu hasa katika maisha ya soka. Jambo hilo limewagusa watu wote wa michezo na wanaendelea kulia hadi sasa.

“Tukiwa kama Atletico Nacional ambao tumeguswa kama binadamu, tunawaomba Conmebol kutoa ubingwa wa Copa Sudamericana na kuwapa Chapecoense kuwa mabingwa wapya wa 2016,” alisema.

Hata hivyo, Conmebol bado hawajatoa tamko lolote juu ya ombi hilo, lakini wengi wanaamini kuwa ombi hilo litasikilizwa.

Klabu ya Corinthians ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini Brazil, imedai kuwa itahakikisha inatoa mchango wao wa kuifanya klabu hiyo iendelee kuwa kwenye ligi kwa misimu mitatu mfululizo bila ya kushuka daraja hadi pale itakapojitegemea.

Mabingwa wapya watetezi wa Ligi Kuu nchini Brazil, Palmeiras pamoja na klabu nyingine kama vile Corinthians, Santos na Sao Paulo, zimedai kuwa zipo tayari kutoa baadhi ya wachezaji wao bure kwa ajili ya kwenda kuisaidia klabu ambayo haina wachezaji kwa sasa.

Klabu ya PSG ya nchini Ufaransa, tayari imetangaza kutoa pauni milioni 40 kusaidia kukijenga upya kikosi cha klabu hiyo ya Chapecoense. Mashabiki wa klabu hiyo juzi walijitokeza kwa wingi kwenye uwanja wao wa soka kwa ajili ya kuwaombea wachezaji wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles