24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Chanzo kifo cha Prince Nelson chagundulika

Prince-Prince-Rogers-NelsonMINNESOTA, MAREKANI

UCHUNGUZI wa kidaktari kutoka jimbo la Minnesota nchini Marekani umebaini kuwa mwanamuziki Prince Nelson, alifariki dunia kutokana na kuzidisha kiwango cha dawa.

Kwa mujibu wa madaktari waliofanya uchunguzi huo wa kifo cha mwanamuziki Prince, wanasema alizidisha kiwango cha dawa za kutuliza maumivu zijulikanazo kama Fentanyl. Dawa hizo zinadaiwa kuwa na nguvu mara hamsini zaidi ya dawa za kulevya za Heroin.

Hata hivyo dawa hizo hutumika wakati wa upasuaji na hasa wagonjwa ambao miili yao ni sugu kwa dawa nyingine za kutuliza maumivu.

Prince alikutwa amefariki dunia Aprili mwaka huu, ndani ya ‘lift’ katika makazi yake huko Minneapolis.

Siku moja kabla ya kifo chake inadaiwa kuwa alikuwa akihitaji msaada kutoka kwa daktari maalumu kutokana na maumivu ya mwili aliyokuwa akiyasikia. Hata hivyo polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi kutokana na kifo hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles