Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital
Kiungo wa Simba, Clatous Chama amejiunga na timu ya RS Berkane ya nchini Morocco ambayo amekwenda nyota wa Yanga Tuisila Kisinda.
Licha ya kwamba Simba haijatoa taarifa kamili ya mchezaji huyo, kuondoka, wachezaji hao wameonekana wakifanya mazoezi na kikosi hicho kinachonolewa na kocha raia wa DR Congo, Florent Ibenge.
Mchezaji mwingine anayeondoka Simba ni Luis Miquissone anakwenda Al Ahly ya nchini Misri, huku Chriss Mugalu naye akihusishwa kujiunga na Far Rabat.
Wanamsimbazi hao wapo nchini Morocco kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.