CHADEMA yashinda Umeya Manispaa ya Ubungo

0
707
meya-wa-ubungo-akizungumza-na-wananchi-nje-ya-ofisi
Meya wa Ubungo Boniface Jacob akizungumza na wananchi nje ya ofisi

Boniface Jacob ambaye ni Diwani wa Kata ya Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, ameshinda nafasi ya Umeya Manispaa ya Ubungo katika uchaguzi uliofanyika leo.

Katika uchaguzi huo ambao mara ya kwanza uliahirishwa, Boniface ameshinda kwa kura 16 kati ya 18 za wajumbe Madiwani wote ambao kati yao, Ukawa walikuwa 15 na CCM 3.

Matokeo hayo yalitangazwa na Katibu wa mkutano Ded Kayombo katika eneo la Kibamba CCM.

Kwa upande mwingine, Kayombo alimtangaza pia Kwangaya Ramadhani (Ukawa) kuwa ni mshindi kwa nafaisi ya Naibu Meya ambaye alipata kura 15 dhidi ya mpinzani wake Abdul Lema wa CCM ambaye alipata kura 3 kati ya 18 na hakuna kura iliyoharibika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here