29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

CHADEMA WALIA RAFU ZA RUSHWA UCHAGUZI MDOGO KIMWANI

CHADEMA-LOGO

Na JONAS MUSHI-DAR ES SALAAM

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya Kimwani katika Halmashauri ya Muleba mkoani Kagera kimedai kuwapo kwa vitendo vya rushwa vinavyofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kampeni zinazondela ili kushinda uchaguzi mdogo wa udiwani unaotarajiwa kufanyika Jumapili.

Chama hicho kinamtuhumu mmoja wa wakandarasi wa Halmashauri ya Muleba (jina tunalo) kuwa juzi alitoa  zaidi ya Sh 80,000 kwa mmoja wa viongozi wastaafu wa Kitongoji cha Njugu ambacho kinakadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya 400.

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (Bawacha) Wilaya  ya Muleba, Adella Thomas aliliambia MTANZANIA kwa simu jana kuwa fedha hizo zimetolewa  zigawiwe kwa wananchi waweze kukipigia kura CCM.

“Huyu mkandarasi anataka (anamtaja jina) anataka CCM ishinde kwa sababu ya kutafuta kupewa tenda kwenye halmashauri. Anataka kutumia udhaifu wa njaa waliyonayo wananchi kuwahonja hizo senti zao ambazo kimsingi ni udhalilishaji kwa wananchi,” alisema Adella.

Mwenyekiti huyo wa Bawacha alizungumzia kampeni zinazoendelea kwenye Kata hiyo ya Kimwani kwa kuviomba vyombo vya usalama hususan jeshi la polisi kuchunguza ujio wa ghafla wa wageni wasiofahamika sawasawa.

“Kuna watu wengi wageni wameingia kwenye kata yetu katika kipindi hiki cha kampeni za lala salama.

“Wengine ukizungumza nao wanajifanya ni wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Halotel wamekuja kwenye promosheni lakini hakuna promosheni yoyote imefanyika hapa Kimwani.

Mmoja wa maofisa wa Takukuru wilayani Muleba ambaye alikataa kuwekwa jina lake gazetini kwa sababu si msemaji rasmi wa taasisi hiyo, aliliambia MTANZANIA kuwa suala hilo limekwishafika mezani kwao na wanalifanyia kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles