33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

KENYA INA CHAKULA CHA KUTOSHA HADI JUNI

Willy Bett
Willy Bett

NAIROBI, KENYA

PAMOJA na makali ya njaa yanayoshuhudiwa katika sehemu kadhaa nchini hapa, Serikali imetangaza kuwa kuna chakula cha kutosha kukidhi mahitaji ya Wakenya hadi Juni.

Waziri wa Kilimo, Willy Bett, alisema juzi kuwa jumla ya magunia milioni 21 ya mahindi yaliyovunwa mwaka jana yatatumika kwa muda wa miezi mitano ijayo.

Alisema hiyo ni pungufu ya magunia milioni tisa, ambayo yatapatikana kutoka vyanzo vingine.

Akizungumza na wanahabari jijini Nairobi jana, Bett alielezea hofu yake kwamba huenda kukawa na uhaba mkubwa wa chakula kuanzia Juni.

“Kwa sasa kuna chakula cha kutosha nchini. Magunia milioni 21 yaliyovunwa mwaka jana yanaweza kutosheleza mahitaji ya Wakenya kwa kipindi cha miezi mitano ijayo,” alisema Bett.

Kwa sasa kaunti 23, hasa katika maeneo ya Kaskazini mwa Rift  Valley, Kaskazini Mashariki, Mashariki na  Pwani zinakabiliwa na baa la njaa, ukosefu wa maji na chakula cha mifugo.

Hali hii imesababisha hofu miongoni mwa wakazi wa maeneo hayo, ambao maisha yao hutegemea mifugo kama kitega uchumi kikuu.

Hali hii imesababisha wabunge kutoka maeneo ya North Rift kuitaka serikali itangaze ukame kuwa janga la kitaifa.

Wakizungumza katika majengo ya Bunge juzi, wabunge hao wakiongozwa na Mbunge wa Tiaty, Asman Kamama, waliitaka serikali isambaze chakula cha msaada na maji kwa wakazi wa maeneo hayo, hasa shule za umma.

Lakini Waziri Bett alisema serikali kupitia wizara ya Kilimo na ile ya ugatuzi, imeanza mchakato wa kusambaza chakula cha msaada kwa Wakenya wanaokabiliwa na baa la njaa.

“Wizara yangu na ile ya Ugatuzi inayosimamiwa na mwenzangu Mwangi Kiunjuri, tumeanza kusambaza chakula kwa Wakenya wanaokabiliwa na baa la njaa kote nchini,” alisema.

Hata hivyo, alikiri kwamba bei ya unga wa mahindi imekuwa ikipanda kwani sasa unauzwa kwa Sh 125 za Kenya (sawa na sh 2,500 za Tanzania) kwa paketi moja ya kilo mbili.

Desemba mwaka jana, paketi hiyo ya unga ilikuwa ikiuzwa kwa Sh 115 (sawa na Sh 2,300 za Tanzania).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles