23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Chadema feki wakamatwa na polisi

chadema fekiNa Asifiwe George, Dar es Salaam

JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni  linawashikilia vijana 10 waliojifanya wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuandamana katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam kwa kile walichodai kwamba ni kupinga hatua ya Dk. Slaa kustaafu siasa kutokana na   Edward Lowassa kujiunga na chama hicho.

Vijana hao waliokuwa wamevaa sare za Chadema walikuwa  wamebeba mabango yenye ujumbe tofauti huku wakiimba wimbo wa‘hatumtaki Lowassa’… ‘hatumtaki Lowassa’.

Akizungumza   Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura  alisema, wanaendelea kuwahoji vijana hao   kujua sababu ya maandamano hayo.

Alisema kutokana na watu hao kukamatwa maeneo mbalimbali ikiwamo makao makuu ya Chadema  watahojiwa kwa   wiki moja.

Wambura alisema polisi hawakuwa na taarifa ya kufanyika   maandamano hayo na hawakutoa kibali chochote kwa vijana hao kuandamana.

Chanzo cha habari kilichokuwa eneo la Morocco wilayani Kinondoni kilisema baada ya hapo yalifika magari matatu (Defender)  yakiwa na polisi ambao walipiga mabomu ya machozi  kuutawanya umati huo.

Mabomu hayo yalisababisha watu hao kukimbia huku na kule   kujinusuru lakini wengine walikamatwa na kufikishwa katika Kituo cha Polisi Osterbay kilichopo wilaya ya Kinondoni,  Dar es Salaam.

Awali taarifa zilizosambaa katika mitandao ya jamii  zilisema   vijana hao ni mkakati uliokuwa umeandaliwa na CCM kuwavalisha  nguo za Chadema   ionekana Lowassa anapingwa ndani ya chama hicho.

Taarifa hiyo ilisema katika mkakati huo unaotajwa kuratibiwa na vigogo kadhaa wa CCM akiwamo mmoja wa wagombea ubunge jijini humo (jina tunalo).

Taarifa hiyo ilisema, “vijana wa CCM watavalishwa nguo za Chadema, wataandamana wakimuunga mkono Dk. Slaa na kumpinga Lowassa”.

Ilidaiwa kuwa maandamano hayo yalitakiwa kuishia Ikulu kwa mapokezi ya makubwa.

Chanzo hicho kilisema mgombea huyo alisuka mkakati huo akidai ni maagizo kutoka uongozi wa juu wa chama na serikali.

Diwani wa ubungo kwa tiketi ya Chadema, Boniface Yakobo, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa

tangu jana usiku chama hicho kilipata taarifa ya kikao kilichofanyika Kariakoo, kingine Ubungo na kiliratibiwa na Didas Masaburi(aliyekuwa Meya wa Dar es Salaam na hivi sasa ni mgombea ubunge wa CCM Ubungo)  ambaye alinunua fulana za Chadema.

Alisema   walizitilia shaka kwa sababu   tangu Chadema ianze haijawahi kutokea kununuliwa tisheti nyingi kiasi hicho.

Kijana huyo alipofuatiliwa ilionekana  amekabidhi fulana hizo kwa Didas Masaburi na (jana) juzi saa 12:00 jioni alionekana akiwa na vijana zaidi ya 100 akifanya nao mkutano, alisema.

Alieleza kuwa baada ya tukio hilo vijana hao walitakiwa kufika Ikulu kushikana mkono na Rais wakielezwa kuwa  kibali kilikuwa kimetolewa na Jeshi la Polisi.

Alisema vijana hao walikuwa wamejipanga katika makundi mawili na saa 5:00 asubuhi kundi la kwanza lilikuwa likitokea Mwenge jingine   Ubungo na kundi la kwanza lilipofika Mkwajuni lilisimama.

“Sisi Chadema tulikuwa tumejipanga na tulikuwa tumewazunguka  lakini kabla ya kuwakamata polisi waliwakamata vijana hao  kabla sisi Chadema hatijawakamata,” alisema na kuongeza:

“Baadhi ya vijana walikamatwa na kupelekwa katika kituo cha polisi lakini baada ya kufika kituoni hapo baadhi yao waliachiwa na kujichanganya na wananchi wa kawaida.

“Wenyewe wamesema hatua hiyo iliratibiwa na ofisi ya CCM Ilala na Kinondoni na   Didas Masaburi.

“Sisi tunawaambia siasa hizi CCM hazina tija, kwa tukio la jana na muendelezo wa leo inaonekana kuna kitu wanakijua na walikuwa wanataka ionekane ni Chadema.

“Tunashukuru umma umetusaidia watu wote waliokimbizwa wamekamatwa na wananchi na   raia… tunamshukuru mtendaji kata kuwahifadhi hao watu ili wasiuawe katika maeneo yale”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles