25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Cecafa yachemka kuipa adhabu Yanga

Katibu wa CECAFA, Nicholas Musonye
Katibu wa CECAFA, Nicholas Musonye

Na Zaituni Kibwana, Kigali

BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limeshindwa kuipa adhabu timu ya Yanga, kwa kosa la kugoma kuwasilisha timu kwenye michuano ya Kombe la Kagame.

Awali baraza hilo chini ya Katibu wake, Nicholas Musonye, lilitangaza kuipa adhabu timu hiyo kwa kitendo chake cha kupeleka timu B katika michuano hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Mwenyekiti wa CECAFA, Leodegar Tenga, alisema hakuna kipengele kinachoweza kuwahukumu Yanga kufuatia kitendo cha kutotuma timu A.

Tenga ambaye aliwahi kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), aliendelea kufafanua kuwa Yanga wangeweza kuadhibiwa kama wangefika katika mashindano hayo na kuonyesha utovu wa nidhamu.

Alisema walichofanya ni kuwaondoa tu kwenye michuano ya mwaka huu, na nafasi yao ikapewa Azam ambao ndio mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Sisi hatuna tatizo na Yanga, ila tuliwasiliana na wanachama wetu wa CECAFA ambaye ni Shirikisho la soka Tanzania (TFF), wao ndio waliipendekeza Azam badala ya Yanga,” alisema.

Hivi karibuni Yanga waligoma kuwasilisha kikosi chao cha kwanza kwenye mashindano ya Kombe la Kagame na kuwafanya CECAFA kuiondoa timu hiyo na nafasi yao kuchukuliwa na Azam.

Azam ambao walipewa uwakilishi wa Tanzania pamoja na KMKM ya visiwani Zanzibar, zimetolewa katika hatua ya robo fainali na makundi katika michuano hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles