22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

CCM yawakana ‘CHAWA’, hawana baraka za chama

*Yasema wanavuruga chama

Na Gustafu Haule, Mtanzania Digital

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa(NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamoud Jumaa, amesema kikundi cha watu wanaojiita “CHAWA” hakina baraka yoyote kutoka chama na hata viongozi wake wa Kitaifa.

Jumaa ametoa kauli hiyo Juni 9, wakati akizumgumza na Viongozi na Wanachama wa CCM katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuimarisha chama na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Hili neno Chawa halina mahusiano na CCM na viongozi wa Taifa wamesisitiza kulisemea  hilo maana watu wanaojihita Chawa wanavuruga chama na kugawa watu na niseme CCM inautaratibu wake ikitaka kufanya jambo lolote lazima liwekwe wazi,” amesema Jumaa.

Jumaa amesema badala ya kujiita Chawa ni vyema wakajiunga au wakaanzisha vikundi maalum vya kuweka na kukopa ili viwasaidie katika kupata kipato cha kusaidia kuendesha familia zao.

“Kuna watu wanatamba sana huko mitaani kuwa wao ni “Chawa” lakini kwa hakika hawana baraka na kiongozi yeyote wa chama wala chama chenyewe ndio maana nasisi tunalisema hadharani kuwa waachane na mambo hayo,” amesema Jumaa.

Amesema kama wana-CCM wa kweli wanatakiwa kutoka na kuyasemea mambo mazuri yaliyofanywa na CCM kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan.

Amesema Rais Samia amefanya mambo makubwa katika kipindi kifupi na anapaswa kuungwa mkono na kumpa moyo ili aendelee kuchapakazi kwa faida ya Taifa .

Aidha, amesema katika kipindi cha miaka miwili ameonyesha kuwa yeye ni kiongozi shujaa na anaweza kufanya mambo makubwa  tofauti na fikra za baadhi ya watu waliodhani Rais Samia hatoweza.

Jumaa amesema mpaka sasa Rais Samia amehakikisha Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere halijasimama na linaendelea kujengwa ambapo mpaka sasa limefikia sehemu nzuri na likikamilika litazalisha megawati 2,115 na hivyo kumaliza changamoto ya umeme nchini.

Mbali na mradi huo lakini pia ipo miradi mingi imetekelezwa ambapo katika elimu amejenga Shule 400 kote nchini zikiwa na jumla ya madarasa 15,000 barabara kubwa zinajengwa, vituo vya afya na zanahati ,madaraja makubwa Kama ya Bugongo- Busisi yanajengwa,na miradi mingine mingi.

Amesema kuna kila sababu ya Watanzania kujivunia uwepo wa Rais Samia kwakuwa amekuwa Rais msikivu mchapakazi na mwenye hekima na amekuwa akifanya mambo ya kulivusha taifa katika masuala ya kimaendeleo.

Akizungumzia uhai wa chama Mjumbe huyo wa NEC, amewataka viongozi na wanachama wa CCM kuimarisha uhai wa CCM na Jumuiya zake kwa kuhakikisha wanakuwepo wanachama hai pamoja na kuendeleza mshikamano wa viongozi na wanachama kwa kufanya kazi kwa umoja na mshikamano wa dhati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles