25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

CCM YAWAANGUKIA WAPIGAKURA KWA NYALANDU

NA GUSTAPHU HAULE -SINGIDA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Singida, kimewaomba wananchi wa Singida Kaskazini kumchagua mgombea wa chama hicho, Justin Monko kuwa mbunge wa jmbo hilo katika uchaguzi unatarajiwa kufanyika kesho.

Ombi hilo lilitolewa jana na Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Jimson Mhagama, alipokuwa akizungumza na wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Itaja.

Alisema mgombea wa CCM anatosha na ndiye anayefaa kuwa mbunge wa Singida Kaskazini kwa kuwa yupo tayari kuwapigania wananchi wake kwa kuwaletea maendeleo.

Aliwataka wananchi hao wa Singida Kaskazini, kutokubali kumpoteza mgombea huyo kwa kuwa chama anachotoka kipo kwa ajili ya kutatua kero zilizopo katika maeneo yao bila ya ubaguzi wa kisiasa, dini wala ukabila.

“Januari 13, mwaka huu wananchi wa Jimbo la Singida Kaskazini tunakwenda kupiga kura za kumchagua mbunge, mimi nawaomba mkamchague Justin Monko kutoka CCM kuwa mbunge wa jimbo hili ili muweze kupata maendeleo zaidi,” alisema Mhagama.

Alisema CCM ikipata mbunge itakwenda kutekeleza ilani yake ya uchaguzi kwa kushirikiana na Serikali ambayo ipo chini ya Rais Dk. John Magufuli ambaye ametokana na chama hicho.

Naye mgombea Monko, alisema kuwa anatambua kero zilizopo katika kata hiyo, hususani ya maji, afya na barabara.

“Naomba kura zenu zote zije kwangu ili tukafanye kazi ya kuleta maendeleo katika jimbo letu, nipo tayari kutumwa na nikatumika kama ambavyo mtapenda nifanye kulingana na changamoto zilizopo,” alisema Monko.

Uchaguzi huo utafanyika baada ya kujiuzulu aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM, Lazaro Nyalandu ambaye alihamia Chadema, huku vyama vingine vinavyowania nafasi hiyo ni Ada-Tadea, AFP, CCK na CUF.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles