25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

CCM yapongeza ushindi wa uchaguzi wa serikali za mitaa, yasisitiza uwajibikaji wa viongozi

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

 Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza kuwa ushindi wake katika uchaguzi wa serikali za mitaa ni dhihirisho la imani ya Watanzania kwa chama hicho. CCM imewataka viongozi waliopata ushindi kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi, kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.

Akizungumza leo, Novemba 29, 2024, jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla, alisema kuwa sasa ni wakati wa kazi baada ya ushindi huo.

“Viongozi walioshinda waliomba utumishi kwa wananchi, na wananchi wamewapa nafasi. Tunataka wawajibike kwa kuomba barua kwa shughuli zao, kufanya vikao vya mapato na matumizi, na kuhakikisha wanatekeleza Ilani yetu,” amesema Makalla.

Makalla alishukuru Watanzania kwa kukipa CCM ushindi na kuwataka viongozi wa ngazi za vijiji, vitongoji, na mitaa kuwahudumia wananchi kwa uadilifu. Amesema mafanikio ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni miongoni mwa sababu za ushindi mkubwa wa chama hicho.

Kuhusu vyama vya upinzani, Makalla alisema migogoro ya ndani imesababisha wananchi kupoteza imani na vyama hivyo. Hata hivyo, amekubali kwamba baadhi ya vijiji vilivyokuwa chini ya CCM vilichukuliwa na upinzani, akisisitiza kuwa hiyo ni sehemu ya demokrasia.

“Nyie mlishuhudia migogoro miongoni mwa viongozi wa vyama vya upinzani. Hali hiyo haiwezi kusababisha ushindi. Sasa ni wakati wa wao kupatana,” aliongeza.

CCM imeahidi kuendelea kuimarisha huduma kwa wananchi kupitia viongozi waliochaguliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles