29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

CCM watakiwa kuacha siasa za vitisho

mgNa Aziza Masoud, Dar es Salaam
MJUMBE wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Khamis Mgeja, amewataka baadhi ya viongozi wa chama hicho kuheshimu haki za wanachama na kuacha siasa za kibabe na kibaguzi kwa kuchunga kauli zao.
Pamoja na hilo, amewataka viongozi hao kutambua hakuna mtu mwenye hatimiliki ndani ya chama hicho ila kila mwanachama ana haki sawa ya kukipigania na kukijenga wakati wote.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mgeja alisema kumekuwa na mambo machafu ambayo yanajitokeza kwa baadhi ya viongozi wa CCM kutuhumiana ovyo pamoja na kutoa kauli nje ya utaratibu wa chama.
Mgeja ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, amewataka viongozi hao kuiga mfano wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa kuwa kiongozi shamba darasa kwa makada wengine wa chama hicho.
“CCM kina utaratibu mzuri sana wa kihistoria uliojengwa kwa heshima, unaoheshimika kwa jamii kwa muda mrefu ndani na nje ya nchi, lakini hivi sasa heshima hiyo inaanza kuchezewa na kumomonyoka polepole na baadhi ya viongozi au kikundi ndani ya chama.
“Kikundi hicho kwa chuki zao binafsi wanaamua kutoa matamko ya mara kwa mara ambayo sio ya chama wala hayahusiani na vikao vya chama kwa sababu ya chuki zao binafsi zisizokwisha, chama ni kikao na maazimio, inashangaza baadhi ya watu wamekuwa wakitoa matamko ambayo siyo maazimio ya vikao,” alisema Mgeja.
Alisema watu hao ni hatari kwakuwa wamekuwa wakitoa matamko yenye ukakasi, maudhi na kichefuchefu na kudai kauli hizo zitakigharimu chama, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.
“Nawaomba hao wanaosema ovyo na kauli za vitisho kwa wana CCM wengine watambue chama hiki si mali ya viongozi bali ni mali ya wanachama na hakuna mwenye hatimiliki na CCM.
“Msitulazimishe tufike mahala kuona chama kilifanya makosa kuwapa dhamana na kuwatwisha jukumu ambalo hamliwezi, dhamana mliyonayo hailingani na maneno mazito ambayo mnayatoa yanayowazidi umri,” alisema Mgeja.
Pia ametoa wito kwa wananchi na wafuasi wa chama hicho kuwapuuza viongozi na wanachama wanaoongea hovyo nje ya maagizo ya vikao halali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles