Anna Ruhasha Mwanza
Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza umelizishwa na kasi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za Sekondari kwa baadhi ya kata zilizopo katika Halmashauri ya Sengerema .
Akizungumza juzi katika ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa miradi hiyo ya kimkakati inayoendelea nchi nzima ,Katibu wa CCM, Wilaya, Muhsin Zikatim licha ya kupongeza pia amesema kuwa chama kimelizishwa na kazi ya ujenzi wa vyumba hivyo katika Jimbo la Sengerema.
Aidha, Zikatim mbali na ukaguzi huo pia ametumia ziara yake kuwahamasisha wanachama wa chama hicho kupitia mikutano ya ndani kutoa elimu kwa jamii ili wapuuze uzushi unatolewa na baadhi ya watu wasiopenda maendeleo kuwa elimu bure haitaendelea ambapo amesema ni uwongo upuuzwe.
“Serikali ya awamu ya sita inaendelea na elimu bure ,kuna baadhi ya watu wanapitapita na kupotosha naomba muapuuze, rais hapa Nyampande ameleta Sh milion 80 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa katika shule ya Sekondari Nyampande,niwaombe tuendelee kumuunga mkono rais wetu, pia ninawapongeza kwa kazi nzuri ya kusimamia miradi hii ya madarasa,” amesema Zikatimu.
Hata hivyo, Diwani wa kata ya Nyampande, George Mwanamalia ameishukuru Ssrikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha kwaajiri vyumba vinne vya Madarasa katika shule ya sekondari Nyampande ambayo ina jumla ya wanafunzi 479 ambapo inategemea kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza 2022 wapatao 301.
“Kata yetu ilipokea sh.milion 80 kwaajiri ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa vinne Kama, mnavyoona tunamalizia na Januari 2022 watoto watapokelewa na hatutakuwa na changamoto ya vyumba vya madarasa na shule yetu itafikisha jumla vyumba 14 vya zamani ni kumi na hivi vinne,” amesema Mwanamalia.
Katibu wa CCM wilaya pamoja na wajumbe wa Sekeretalieti ya wilaya wanaendelea na ziara kata kwa kata na kuzungumza na baadhi ya viongozi wa chama hicho ngazi ya kata katika na kupokea taarifa za ute zelezaji wa ilani.