26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

Balozi Elsie akutana na Meya wa mji wa Dallas

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

BALOZI wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Elsie Kanza, amefanya mazungumzo na  Meya wa Mji wa Dallas, Meya Eric Johsnon, kuzungumza  na Jumuiya ya Watanzania (Diaspora) waishio Marekani na Mexico.

Mazungumzo kati ya Balozi Kanza na Meya Johnson yalilenga katika kuimarisha uchumi wa kidiplomasia hususan sekta za utalii,biashara na uwekezaji ambapo amemuomba kuwahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji  kuwekeza Tanzania kutokana na uwepo wa fursa nyingi.

Amesema mazingira ya biashara na uwekezaji yakiwa yameboreshwa kwa kuondoa kodi kero tangu Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan uingie madarakani.

Katika Mkutano na Watanzania waishio Marekani na Mexico, amezungumzia juu ya namna ya kutangaza fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zilizopo Tanzania pamoja na kuweka mikakati ya kuwavutia watalii wengi kwenda Tanzania kutembelea vivutia mbalimbali vya uwekezaji.

Pia mazungumzo hayo na Watanzania, lengo ni kujitambulisha katika jumuiya hiyo na kujadiliana masuala mtambuka kuhusu maendeleo ya Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles