32.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

CATALONIA KUJITANGAZIA UHURU

BARCELONA, HISPANIA

CATALONIA inatarajia kutangaza uhuru wake kutoka Hispania siku chache zijazo, kwa mujibu wa kiongozi wa eneo hilo, Carles Puigdemont.

Katika mahojiano yake ya kwanza tangu ifanyike kura ya maoni Jumapili iliyopita, Puigdemont alisema Serikali yake itachukua hatua mwishoni mwa wiki hii au mwanzoni mwa wiki ijayo.

Kwa upande wake, Mfalme wa Hispania, Felipe VI, amasema waandaaji wa kura hiyo walikiuka sheria na kwamba hali ya sasa nchini humo si nzuri akitaka kuwapo umoja.

Maelfu ya watu wa Catalonia wamekuwa wakigoma kupinga ghasia za polisi wa Hispania wakati wa kura, ambapo takribani watu 900 na polisi 33 walijeruhiwa.

Akizungumza wakati wa mahojiano na BBC, Rais wa Catalonia, Puigdemont, alisema Serikali yake itachukua hatua mwishoni mwa wiki hii au mwanzo wa wiki ijayo.

Alipoulizwa kuhusu ni kipi atakifanya ikiwa Serikali ya Hispania itaingilia kati na kuidhibiti Serikali ya Catalonia, Puigdemont alisema kuwa yatakuwa ni makosa ambayo yatabadilisha kila kitu.

Puigdemont alisema kwa sasa hakuna mawasiliano kati ya Serikali mjini Madrrid na utawala wake huku akipinga taarifa ya Tume ya Ulaya ya Jumatatu kuwa kile kinachoendelea Catalonia ni masuala ya ndania ya Hispania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles