26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

CASSO AFUNGUKA TATTOO YA ROSE NDAUKA

MSANII wa Bongo Fleva, Casso ambaye yupo chini ya lebo ya Ndauka Music inayomilikiwa na mwigizaji, Rose Ndauka amesema sababu zilizofanya achore tattoo yenye jina la mrembo huyo kwenye mkono wake wa kulia ni mapenzi aliyonayo kwa bosi.

Casso ameliambia Show Biz kuwa Rose Ndauka ana roho ya kipekee na ni rafiki ambaye Mungu amemleta kwenye maisha yake kwa kusudi maalumu hivyo hana budi kumheshimu na kumuweka kwenye kumbukumbu zisizofutika.

“Nimechora tattoo ya jina lake kwenye mkono wangu ili iwe kumbukumbu, amenisaidi kimuziki na kimaisha hivyo hata siku moja nikiwa na mafanikio niweze kumuonyesha mwanangu tattoo hii kama ni mtu aliyefanya mimi nifanikiwe,” alisema Casso ambaye yupo mbioni kuachia wimbo wake mpya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles