CARDI B KUTUMIA BILIONI MOJA KWA AJILI YA HARUSI

0
857

LOS ANGELES, MAREKANI


MWANAMUZIKI wa Rap kutoka Marekani, Cardi B, amepanga kutumia dola milioni moja ambayo ni sawa na Sh  bilioni mbili za Tanzania, katika sherehe yake ya harusi itakayofanyika hivi karibuni.

Mwanamuziki huyo anatarajia kufunga ndoa na mwanamuziki wa Rap, Kiari Kendrell Cephus maarufu kama Offset, kutoka kwenye kundi la Migos la Marekani.

Cardi ambaye alivishwa pete ya uchumba Oktoba mwaka huu, alisisitiza kwamba matumizi yake katika harusi hiyo hayataingiliana na mumewe mtarajiwa Offset.

Akizungumzia siku ya harusi yao, Cardi B alisema: “Tutatumia fedha nyingi, sidhani kama ni sawa kumuacha Offset kulipa kila kitu, nahisi nitalipa zaidi yake kwani gauni langu huenda likagharimu dola 50,000,” alisema Cardi B.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here