28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Card B ang’ara tuzo za BET

Los Angeles, Marekani

Wasanii mbalimbali na wanamichezo walijawa na furaha baada ya kutajwa wao ndiyo washindi katika vipengele mbalimbali katika tuzo za BET, mwanadada Card B akiongoza kwa kuchukua tuzo mbili kwa mpigo.

Tuzo hizo amabazo hutolewa kila mwaka huwatunuku pia tuzo za heshima wasanii ikiwa ni kuheshimu na kutambua mchango wao katika sanaa ya muziki duniani na mwaka huu tuzo ya heshima ilienda kwa Mary J Blige ambaye alibubujikwa na machozi wakati msanii Rihanna aliyepewa nafasi ya kumkabidhi tuzo hiyo akimshukuru na kumtaja kama mwanamke shupavu na kuchangia uthubutu kwa wanawake wengi.

Tuzo hizo zilitolewa Juni 23, Los Angeles, Marekani na mwanadada Card B aliibuka mshindi wa tuzo mbili, ambapo alishinda tuzo ya Albamu Bora ya Mwaka (Invasion of Privacy) na Msanii Bora wa Hiphop wa Kike na alikuwa akiwaniakatika vipengele saba tofauti.

Msanii Burna Boy kutoka nchini Nigeria, alishinda tuzo ya  Best International Act huku tuzo ya Best New international Act ikichukuliwa na Sho Madjozi wa Afrika Kusini

Tuzo za Filamu zilienda kwa Michael Jordan kama Muigizaji Bora wa Kiume na Muigizaji Bora wa Kike ilichukuliwa na Regina King wakati  BlacKkKlansman ikichukua tuzo ya ilamu Bora.

Katika tuzo za BET pia kulikuwa na kipengele cha michezo ambapo Mwanamichezo Bora wa Kike alichukua Serena William na Mwanamichezo Bora wa Kiume imechukuliwa na Stephen Curry.

Katika kumuenzi msanii Nipsey Hussle  aliyefariki kwa kupigwa risasi Machi 31 mwaka huu, alipewa tuzo ya  Mwanamuziki Bora wa Hiphop marehemu ambapo aliwabwaga 21 Savage, Drake, J. Cole, Meek Mill na Travis Scott.

Mwanamuziki Bruno Mars allibuka mshindi wa tuzo ya Msanii Bora wa Kiume  wa Pop na R&B na Msanii Bora wa Kike wa Pop na R&B ilichukuliwa na Beyonce.

Aidha tuzo ya Kundi bora la Mwaka ilichukuliwa na Migos ambalo linaunfwa na wasanii watatu Quavious Keyate Marshall (Quavo), Kiari Kendrell Cephus (Offset) na Kirshnik Khari Ball (TakeOff).

Tuzo ya Video Bora ya Mwaka ilichukuliwa na This is America ya msanii Childish Gambino huku Muongozaji Bora wa Video ikichukuliwa na Karena Evans.

BET pia hutolewa kwa wasanii wacahanga manpo kwa mwaka huu tuzo ya Msanii anayechipukia ilichukuliwa na Lil Baby na tuzo msanii mdogo zaidi ilichukuliwa na Marsai Martin.

Msanii Snoop Dogg alishinda tuzo ya Wimbo Bora wa Dini Na Unaohamasisha kupitia wimbo wake wa  ‘Blessing Me Again’ aliomshirikisha Rance Allan huku tuzo ya Wimbo Bora wa kushirikiana ikichukuliwa na Travis Scott kupitia wimbo wake ‘ wa ‘Sicko Mode’ aliomshirikisha Drake.

 BET pia hutoa mafasi kwa watazamaji kuchagua video bora na kwa mwaka huu tuzo ya Chaguo la Watazamaji inayodhaminiwa na Coca Cola imechukuliwa na Ella Mai na wimbo wake wa ‘Trip’ na tuzo ya ‘BET HER’ imechukuliwa na wimbo wa ‘Hard Place’ ya H.E.R.

Aidha tuzo hizo ziliongozwa na muigizaji Regina Hall na wasanii waliotumbuiza usiku huo ni Card B, Meek Mill, Mary J Blige, Migos, John Legend, Lil Bbaby, DJ Khalled ambaye alipanda jukwaan na timu yake kuimba wimbo wa Higher wakiwa wamevalia mavazi meupe kama ishara ya kumkumbuka marehemu Nipsey Hussle aliyeshirikiana naye katika wimbo huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles