26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

TAEC, IAEA wajadili sheria, udhibiti madini ya urani

Mwandishi Wetu, Arusha

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa kushirikiana na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) wameanza mkutano ambao pamoja na mambo mengine utajadili miundombinu ya sheria iliyopendekezwa na udhibiti wa madini ya urani.

Mkutano huo wa siku tano ambao pia umeshirikisha nchi wanachama wa IAEA Kanda ya Afrika zinazodhibiti usalama wa mionzi umeanza leo jijini Arusha.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tume hiyo, Peter Ngamilo amesema; “Lengo kuu la mkutano huu ambao umehudhuriwa na washiriki 27 ni kujadili na kutoa miongozo kulingana na viwango vya usalama kwa wasimamizi wa nchi za wanachama wa Afrika juu ya utoaji wa leseni na ukaguzi wa shughuli za mzunguko wa uzalishaji wa madini ya urani.”

Awali akifungua mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Injinia John Ngatunga, amewataka washiriki wote kufanya majadiliano ambayo yatasaidia kuelewa miundombinu iliyopendekezwa ya sheria na udhibiti wa madini ya urani na majukumu ya washirika wengine wa udhibiti katika ngazi za kitaifa na kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles