25.4 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Calisa apata shavu la Condom, kukinukisha Zanzibar

Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya DKT lnternational Tanzania, wameandaa shindano la uendeshaji baiskeli ‘Cycle for HIV 2022’ visiwani Zanzibar, kwa lengo la kuhamasisha jamii kujikinga na mambukizi ya ugonjwa wa ukimwi pamoja na mimba zisizo tarajiwa.

Kampuni hiyo ambayo imewatambulisha Mwanamitindo Calisah Abdulhamidu ‘Calisah’ kuwa balozi wa bidhaa yao ya Bull Condom, Miss Arusha 2020, Tamia Ally kuwa balozi wa Kiss condom na Dj Kidy Lax kuwa balozi wa Fiesta Condom na muigizaji, Magdalena Munisi kuwa balozi wa vidonge vya kuzuia mimba (Trust).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumatano Juanuari 26, 2022 Afisa Masoko wa Kampuni hiyo, Farida Rubanza, amesema shindano hilo litahusisha watu wenye umri kuanzia miaka 18 washindi wa nne watapata nafasi ya kwenda Zanzibar kuanzia 18 hadi 20 kwa ajili ya kupatiwa uwelewa zaidi wa bidhaa hizo pamoja na kushiriki kampeni hiyo.

“Nipende kuiomba jamii kuungana nasi katika kampeni hii ya uhamasishaji wa kujikinga afya zetu kwa kutumia kinga ili kufikia malengo kwa ambaye atapenda kushiriki katika shindano hili anaweza kupitia katika kurasa za mitandao ya kijamii ya bidhaa hizo ili kupata maelekezo zaidi,” anasema Rubanza.

Mmoja wa mabalozi hao Calisa akiongea kwa niamba ya wenzake ameishukuru kampuni hiyo kwa kuwaamini katika kuhamasisha jamii kujali afya zao kwa kitumia kinga.

“Niwaombe vijana wenzangu kuacha kuuza mechi kwa starehe ya mara moja kuacha kufanya tendo la ndoa sio rahisi hivyo inatupasa kutumia kinga ili kulinda afya zetu,” amesema Calisa.

Ameongeza kuwa mbali na ugonjwa wa ukimwi yapo magonjwa ya zinaa ambayo yana sababishwa na ngono zembe ikitokea mtu amepata yanachelewesha mafanikio kwa kuchukua muda mrefu kujiuguza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles