23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘Watoto wa kike wanaongoza kwa kufanyiwa ukatili’-Dk. Gwajima

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk.Doroth Gwajima amesema takwimu zinaonesha waathirika wakubwa wa vitendo vya ukatili kwa upande wa watoto ni asilimia 70 ni wasichana.

Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wake wote itaendelea kuimarisha utekelezaji wa afua zenye kuhamasisha kuzuia na kushughulikia aina zote za ukatili ili kuhakikisha jamii ya kitanzania inafurahia haki ya kuishi.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumanne Januari 25,2021 wakati alipofanya ziara katika makao ya watoto na makazi ya wazee  cha Home Of Love and Joy kilichombo Hombolo jijini hapa.

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk.Doroth Gwajima.

Katika ziara hiyo, Dk. Gwajima alikuwa ameongozana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mwanaidi Ally Khamis, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk.Zainabu Chaula na Amon Mpanju na wataalamu wa Wizara hiyo.

Waziri Gwajima amesema kuwa, watoto wanapokuwa wanaishi kwenye mazingira hatarishi pamoja na changamoto nyingi pia wanakutana na ukatili mkubwa.

Aidha, ukatili wa majumbani ni sababu mojawapo inayowafanya watoto wakimbilie mitaani na matokeo yake wanakutana na aina zingine za ukatili na mazingira hatari zaidi.

Amesema takwimu zinaonesha waathirika wakubwa wa vitendo vya ukatili kwa upande wa watoto asilimia 70  ni wakike.

“Pamoja na serikali na wadau wake kuendelea kupambana kuzuia ukatili pia inatoa huduma kwa wahanga wa ukatili ikiwemo huduma ya kisheria ambapo kwa mwaka 2020/21 mashauri 3,889 yamepelekwa mahakamani na 1,504 yametolewa hukumu na mengine kazi inaendelea,”amesema Dk. Gwajima.

Amesema mbali na ukatili kwa watoto, hata watu wazima wanafanyiwa ukatili ambapo wanawake wanatengeneza asilimia 96 ya wanaoathirika.

“Kwa ujumla wake ukatili kwa mtu yeyote haukubaliki, hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau wake wote itaendelea kuimarisha utekelezaji wa afua zenye kuhamasisha kuzuia na kushughulikia aina zote za ukatili ili kuhakikisha jamii ya kitanzania inafurahia haki ya kuishi,” amesema Dk. Gwajima.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mwanaidi amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameona umuhimu wa kuanzisha wizara hiyo kwa kuwa ni eneo pana, hivyo wameunda timu ya kutembelea vituo mbalimbali ambavyo vinalea wazee na watoto lengo ni kujua kwa undani changamoto ambazo wanakutana nazo ili waweze kuzitatua.

“Upendo unahitajika sana ndio maana Mwalimu Nyerere na Karume waliona umuhimu wa kuanzisha vituo hivi. Maafisa Maendeleo ya Jamii kwa sasa hawana kazi sasa kazi imeanza Rais anataka kuona tunafanya kazi kutembea na kuona uhalisia,”amesema.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk.Chaula amesema huo ni mwendelezo ziara ya kutembelea vituo vya kulelea watoto na wazee ambapo walianza Januari 17, mwaka huu Kikombo na Kijiji cha Matumaini.

Kwa upande wake, Sister Radience wa Makao ya Watoto na Makazi ya Wazee ya Home Of Love and Joy, amesema lengo la kuanzishwa kituo ni kuhudumia kutoa huduma kwa maskini bila ya  kubagua dini wala ukabila ambapo walengwa hupatiwa huduma zote bure.

Amesema wanakabiliwa na changamoto za gharama kubwa za uendeshaji wa kituo malipo kwa ajili ya umeme na wale ambao wanaumwa hivyo wameomba wapatiwe Solar pamoja na bima ya afya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles