29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

CAG Profesa Assad aanza kukunjua makucha

Profesa Mussa Juma Assad
Profesa Mussa Juma Assad

NA ELIYA MBONEA, ARUSHA

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Professa Mussa Juma Assad, ameanza kukunjua makucha kwa kuwaonya watu wanaochanganya siasa na biashara.

Profesa Assad alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa mwaka wa wahasibu na wakaguzi zaidi ya 3,000 unaoendelea kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) mjini hapa.

“Kuna kitu nakiita kuchanganya siasa na wafanyabiashara, nawaambia lazima utenganishe mwingiliano binafsi wa kimaslahi, mnachotakiwa kufanya zingatieni taaluma yenu.

“Kama utaona uamuzi unaoufanya unakinzana na maslahi yako binafsi, kimsingi unatakiwa usifanye lolote,” alisema.

Alisema tatizo kubwa lilipo nchini linatokana na watu wenye maslahi binafsi kuingia kwenye vyombo muhimu vya uamuzi ambapo baadaye husababisha matatizo makubwa.

“Jambo hili itabidi tulipige vita kwa kadiri tutakavyoweza ili watu au viongozi waweze kufanya uamuzi bila kuangalia maslahi yao,” alisema Professa Assad.

Akizungumzia taaluma ya uhasibu, Profesa Assad alisema taifa linahitaji kuwa na wahasibu na wakaguzi wenye weledi mkubwa zaidi ili kufikia malengo waliyojiwekea.

“Hapa si weledi peke yake, bali watu hawa wanatakiwa mwenendo wao uendane na mipango ya uhasibu na ukaguzi duniani, wanapaswa kujifunza mambo mapya kadiri siku zinavyobadilika.

“Taaluma yetu inataka tuwe tunajifunza mambo mapya kila siku, naamini tukifanya hivi basi malengo yetu yatafika pale tunapopahitaji,” alisema.

Katika hatua nyingine, CAG amewaahidi Watanzania kutekeleza na kusimamia majukumu yote yaliyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Nashukuru nimeingia kwenye ofisi ambayo tayari Watanzania wana imani nayo, nafikiri sehemu kubwa ambayo tunatakiwa kutizama ni kurekebisha sehemu ya mtazamo wetu wa maisha ili tuendelee kuaminiwa,” alisema.

Awali akifungua mkutano huo, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, aliwataka wahasibu na wakaguzi kuwa makini katika maeneo waliyopewa kuyafanyia kazi hususani rasilimali za taifa.

Alisema moja ya rasilimali ambayo itakuwa inafanyiwa tathimini na CAG ni kwenye masuala ya mafuta, gesi, oil, madini na misitu.

“Hata kwa nchi zilizoendelea, fani hizi ni maalumu kwani unaweza kumkuta mtu ni mhasibu na mkaguzi katika masuala ya oil na gesi. Ndiyo maana nasema ili kulinda rasilimali zetu kwa makini lazima sisi wenyewe tuwe na uzalendo,” alisema Malima.

Profesa Assad aliapishwa wiki iliyopita na Rais Jakata Kikwete, akichukua nafasi ya Ludovick Utouh aliyestaafu kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Huwezi kuwwajibisha mafisadi wakati wewe mwenyewe ni fisadi, unahitajimtu msafi. Kiongozi ambaye aliweza kuwawajibisha viongozi wezi ni mmoja tu Tanzania nzima hadi leo, naye ni Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu JK Nyerere, wengine wote waliofuata, kama Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete ni ubabaishaji na ubatili mutpu. Tanzania inabhitaji mabadilikoya kichama, ccm lazima iondoke kama tutanataka kuondoa ufisadi. CCM ni serikali yakifisadi, sasa unategemea nini? Ufisadi ni mfumo ndaniya serikali ya ccm, wakiacha ufisadi hawawezikuwa madarakani leo au kesho, kwa hivi dawa pekee ya ccm kuendelea kutawala ji kwa njia ya ufisadi, rushwa, uwongo, ubabe na wizi, hayo watanzania lazima myajue badala ya kujifanya hamujui ccm. Na hivi hata katiba pendekezwa ni yakulinda mafisadi na wezi, kwa hivi katiba hii haikubaloiki, ni lazima itupiliwe mbali kabisa, nikitanzni chamauti ya watanzania wa leo na kesho. Watanzania kazi kwenu kuamua kuishi au kufa,chanzo cha matatizo yote nchini Tz ni “CCM” chama cha Mafisadi. Dawa ni kila mtanzania kuweka nia ya kutokukipigia kura kuanzia serikali ya mtaa hadi uchaguzi mkuu 2015 bila kujaliitikadi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles