26 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

CAG aombwa kukagua miradi Sengerema

Na Sheila Katikula, Mwanza

Mbunge wa Sengerema, Hamis Tabasamu amemuomba Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere kutembelea miradi ya maji iliyopo kwenye wilaya hiyo ili awezekuwa huru katika uongozi wake.

Akizungumza wakati wa kikao cha kwanza cha bodi ya barabara ya mkoa wa Mwanza kwa mwaka wa fedha 2020/2021, Tabasamu amesema miradi ya Maji bado ina ubabaishaji kwenye jimbo hilo.

Amesema mradi wa maji wa Buyagu umeanza mwaka 2014 na umegharimu Sh bilioni Sh 1.7  na fedha zimeliwana, mradi wa Katunguru ulianza mwaka 2019 na umegharimu Sh milioni 730 na haijakamilika.

Tabasamu amesema mradi wa maji wa Nyamazugo umegharimu Sh bilioni 23 na mpaka sasa  haujakamilika takribani kwa miaka mitatu.

Amesema mradi wa Nyampande ulianza march mwaka 2019 na ulitakiwa ukamilike Oktoba mwaka huu lakini haujakamilika na umetumia  Sh bilioni 1.35 na mradi wa Taruka buswabangili kwani yote imekwisha muda wake.

“Miradi ya maji iliyopo Sengerema niya ujambazi tumezungumza na CAG na watu wake na leo hii nimezungumza na kwenye kikao hiki tumekubaliana  na  Suwasa, mwauwasa na Ruwasa tunataka  tuirudie kuikagua  kwani inatesa wananchi wakiskia  Sh bilioni 1.3 na bilioni 1.6 alafu hakuna maji wanaumia sana.

“Kama tungekuwa tumechimba visima tukaacha miradi hii ya ujambazi kwani wananchi hawanashida na miradi ya mabomba ila yanatakiwa yapelekwe kwenye maeneo ya mjini lakini vijijini  mtu anataka achote maji kwenye kisima naende nyumbani kwake watu wanatafuta  kisima cha Sh milioni 30 hakipo, nafikiri hili tutamshauri Rais Dk. John Magufuli kwani tunaona watu wanaendesha magari kwa pesa zetu za maji hadi roho inaima.

“Kuna mradi wa maji Nyamazugo Sengerema Sh bilioni 23, mradi huu unadaiwa unamiaka mitatu umeshindwa kulipa deni la Sh milioni 300 la Tanesco, mradi Sengerema Nyampande wa Sh bilioni 1.35, Rubungo ngoma A umecheleweshwa kuanza kwake tunaona Watu wamejenga tu hatujui fedha zimekuja kiasi gani ni mradi wa bilioni 4.6,  Tabaruka 

“Sengerema kuna mradi wa Busubwangili wa Sh milioni 400 wa Katungulu  Nyamtelela wa Sh milioni 730, Chabanda Kasingamile wa Sh bilioni 1.35 yaani hadi kichefu chefu kutaja  ee…Mungu wee naomba CAG aje haraka ili niwe huru katika uongozi wangu,” amesema Tabasamu.

Ameongeza kuwa katika utekelezaji wa maendeleo ya miradi ya barabara, kuna changa moto kwa wakala wa barabara (Tanroad) katika utoaji wa taarifa za miundo mbinu.

Hata hivyo ameiomba Tanroad  kuchora ramani za barabara ili waweze kujua ni aina gani za barabara zinazojengwa katika maeneo yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles