29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Byabato atangaza kiama kwa watusmishi wasio waaminifu Tanesco

Na Nyemo Malecela, Kagera


Naibu Waziri wa Nishati, Adv. Steven Byabato, ametangaza mwisho wa watumishi wasio waaminifu wanaolichafua Shirika la Umeme Tanesco kwa kuwaomba wananchi rushwa ili wawaunganishie umeme.

Byabato amesema hayo jana katika ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya umeme na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa Jimbo la Bukoba Mjini kuhusu nishati hiyo wakati akiwa ameambatana na wafanyakazi wa Tanesco kutoka Makao Makuu Dodoma, Kanda ya Ziwa na mkoani Kagera.

Naibu Waziri wa Nishati na mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Adv Steven Byabato (wa tano kushoto) akizungumza na wananchi wa kata Kashai jimboni humo wakati alipoongozana na watumishi wa tanesco Makao Makuu Dodoma Kanda ya Ziwa na mkoani Kagera kukagua miundombinu ya umeme jimboni humo pamoja na kusikiliza kero za wananchi.

Baada ya kufanya ziara hiyo ya siku mbili na kuzunguka katika mitaa mbalimbali iliyoko katika kata za Nyanga, Buhembe, Kashai na Nshambya alisema “wakati umefika wa shirika la Tanesco kutoendelea kuchafuliwa na watu wachache ambao sio waaminifu,” amesema Byabato.

Kufuatia malalamiko ya wananchi kwa watumishi wa shirika hilo, Byabato amewaagiza viongozi wa Tanesco nchini kuwachukulia hatua madhubuti watendaji wote wanaolihujumu shirika hilo kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa wanapotoa huduma kwa wataje.

Byabato alifikia hatua hiyo baada ya wananchi kumweleza kuwa wapo watumishi wa Tanesco wanaotumwa mitaani kuwahudumia wamekuwa wakiwaomba rushwa kwa madai kuwa shirika hilo halina dhana za kutosha za kuwawezesha kuwafikishia umeme katika nyumba zao.

Miongoni mwa zana zinazodaiwa kutumiwa na watumishi hao kuombea rushwa ni pamoja na nguzo za umeme, nyaya za umeme zinazotoka kwenye nguzo na kuingiza umeme kwenye nyumba na mchakato wa kujaza fomu za maombi, kufanyiwa ukaguzi, kupewa control number na kupewa mita.

“Nataka niwahakikishie kuwa Serikali imejipanga kufikisha umeme kwa wananchi kwa wakati bila kuwabughuzi hivyo kauli za kuambiwa na watumishi wa Tanesco kuwa mnatakiwa mjiongeze, mueleweke ndipo mpatiwe umeme nimezipokea na nitazifanyia kazi na zitakoma kuanzia sasa.

“Kama kweli Tanesco inakuwa ina upungufu wa dhana hizo mbona mnapoeleweka na kujiongeza kwa kuwapatia shilingi 15,000 nguzo na nyaya zinapatikana, zinatoka wapi wakati walishasema shirika halina dhana hizo? Au mkishatoa kiasi hicho cha fedha waya unarefukaje hadi kufika kwenye nyumba wakati walishawaambia ni mfupi?,” amehoji Byabato.

Naibu Waziri wa Nishati na mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Adv Steven Byabato akiwagawia vitumbua wananchi na viongozi wa tanesco Makao Makuu Dodoma Kanda ya Ziwa na mkoani Kagera wakati wa ziara yake katika Jimbo hilo kwa ajili ya kukagua miundombinu ya umeme na kusikiliza kero za wananchi.

Wakati huo huo Byabato amekemea tabia ya Tanesco kuchelewa kupeleka wakaguzi ‘servery’ kwa wateja wanaojaza fomu za kuomba umeme na wakishapimiwa bado wanacheleweshwa kupewa control number kwa ajili ya kulipia hiyo bei ya shilingi 27,000 na baada ya kulipia wanachelewa kuunganishiwa umeme.


Pia Byabato amewaambia wananchi hao kuwa kufikia Novemba mwaka huu kila mwananchi anatakiwa kuwa ameunganishiwa umeme nyumbani kwake kwani gharama ya kuunganishiwa umeme majumbani kwa sasa ni Sh 27,000.

“Serkali ya awamu ya sita tayari imeweka kiwango cha matumizi ya unit moja ya umeme italipiwa kwa Sh 100 kwa wale wasiozidi matumizi ya unit 75 kwa mwezi wakati huo ikileta miradi mipya ya umeme wa REA 3 mzunguko wa pili na mradi ya maeneo ya mijini unatarajia kuanza hivi karibuni.

Hivyo nawaomba wananchi kutunza miundombinu ya umeme kwa kuacha tabia ya kuchoma moto mapori na kusababisha kuungua kwa nguzo za umeme kwani serkali imetumia gharama kubwa kuweka miundombinu hiyo.

“Zaidi ya shilingi bilioni tatu zimeshatengwa kwa ajili ya malekebisho mbalimbali ya miundombinu ya Mkoa wa Kagera ili kila mwananchi atakayepata umeme uwe wa kutosha, gharama nafuu na unaotabirika.

“Wakati huo mwenyekiti wa mtaa wa Bushaga kata Kashai, Richard Rugaika aliiomba serikali kupunguza gharama za kufanyiwa ukaguzi wa miundombinu ya umeme ndani ya nyumba kwa ajili ya kuwekewa umeme kama ilivyopunguza gharama za kuunganishiwa nishati hiyo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles