28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Abiria ambaye hajavaa barakoa asipakiwe

Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesisitiza na kuwataka wamiliki na LATRA kusimamia level seat na abiria wote kuvaa Barakoa wanapopanda kwenye vyombo vya usafiri.

Amewataka wamiliki wa vyombo hivyo kuwaelekeza madereva na makondakta kuepuka kubeba abiria asievaa barakoa pamoja na kujaza abiria wengi kwenye gari.

Akizungumza wakati wa kikao na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa kupitia tathimini ya utekelezaji wa mwongozo ukiotolewa na Wizara ya Afya juu ya kujikinga na Corona na kuendelea kusitiza abiria kukaa level seat.

“Kumekuwa na ulegevu wa usimamizi kwenye baadhi ya maeneo ambapo nimetoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Wilaya na LATRA kuhakikisha wanasimamia ipasavyo mwongozo wa Wizara ya Afya.”

“Kutokana na changamoto za usafiri kwa wanafunzi, naruhusu Daladala kubeba Wanafunzi watano watakaosimama lakini kwa kigezo cha wanafunzi hao kuwa wamevaa Barakoa.” amesema Makalla

Aidha Makalla ameendelea Kusisitiza Wananchi kuepuka Mikusanyiko isiyokuwa na lazima na Kama ikitokea Kuna ulazima taratibu zote za kujikinga zizingatiwe.

“Nimefurahi kuona Wananchi wamekuwa na mapokeo makubwa ya kupokea chanjo ambapo kwa Mujibu wa Mganga mkuu wa Mkoa huo adi kufikia Jana tayari Wananchi 10,000 wamefanya booking na wanahofia chanjo zitawahi kumalizika,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles