23 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Polisi yawaonya wanasiasa

Na Allan Vicent, Tabora 

JESHI la Polisi Mkoa wa Tabora, limewaonya  wanasiasa wanaotetea au kulinda watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu kuacha mara moja tabia hiyo vinginevyo nao watakamatwa kama wahalifu wengine.

Onyo hilo limetolewa jana na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Safia Jongo, alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio ya oparesheni waliyofanya dhidi ya uhalifu na wahalifu  mbele ya waandihi wa habari.

Amesema wanasiasa wanatakiwa kufanya kazi zao kwa manufaa ya jamii na sio kutetea au kulinda watu au kikundi cha watu kinachojihusisha na vitendo visivyokubalika miongoni mwa jamii ikiwemo kufanya uhalifu.

Amebainisha kuwa serikali haijalala usingizi, ipo macho na Jeshi la Polisi lipo imara kuhakikisha wale wote wanaofanya vitendo visivyokubalika kwa mujibu wa sheria ikiwamo uhalifu wa aina yoyote ile wanakamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki.

‘Sina muhali na mhalifu, yeyote atakayebainika kufanya vitendo vya namna hiyo atashughulikiwa kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria pasipo kupepesa macho, tumejipanga vizuri’, alisema.  

Kamanda Safia amewataka wale wote wanajiohusisha na uhalifu kuacha mara moja tabia hiyo, alitoa wito kwa wanasiasa na jamii kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili ukomeshwe.  

Aidha ameitaka jamii mkoani humo kuendelea kuchukua tahadhari ya Ugonjwa wa Corona (UVIKO 19) kwa kuvaa barakoa, kunawa mikono na sabuni kwa maji tiririka na kutumia vitakasa mikono ikiwemo kujiepusha na mikusanyiko isiyo ya lazima ili kujilinda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles