30.3 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

BUWASA yatenga Milioni 3 kuokoa upotevu wa maji

Renatha Kipaka, Bukoba

Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira Bukoba(BUWASA) imesema ili kuokoa upotevu wa maji imekuwa ikitenga Sh milioni 3 kila mwezi kutoka makusanyo ya ndani kwa ajili ya kubadili mabomba chakavu.

Hayo yamebainishwa jana na Afisa Matengenezo na Usambazaji wa maji Bukoba, Kuboja Charles ambapo amesema hatua hiyo ni baada ya mamlaka kupokea taarifa ya kupasuka kwa mabomba na kubaini upotevu wa maji.

Hata hivyo, Charles amesema timu ya mafundi kutoka Kanda ya Kashai, mjini Kati na Ukanda wa Kijani walitembelea mitaa na kubaini upotevu mkubwa wa maji kwa asilimia 47 hadi 49 katika uzalishaji.

“Tumebaini upotevu wa maji unaosababisha na uchakavu wa mabomba yanayopasuka ambayo yalikuwa yakiwekwa na wateja weyewe.

“Hivyo katika kukabiliana na hali hiyo BUWASA imelazimu kutumia makusanyo ya ndani kila mwezi kwa kutenga Sh milioni 3 kwa ajili ya kufanya maboresho ya miundombinu mtaa kwa mtaa,” amesema Charles.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles