27.4 C
Dar es Salaam
Thursday, December 9, 2021

BUWASA yaongeza huduma za maji kwa wananchi

Renatha Kipaka, Bukoba

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA) imefanya upanuzi wa huduma ya maji kwa Wananchi wa wilaya ya Missenyi, Karagwe Kyerwa Ngara, Muleba, Bukoba, na Biharamu Mkoani Kagera kwenye maeneo ambayo yanatatizo la upatikanaji maji.

Kauri hiyo ilitolewa na Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka hiyo Mjini Bukoba, John Sirati amesema hatua hiyo ni kutekeleza na kusimamia miradi ambayo imeongezwa na wizara ya maji.

Hata hivyo, amesema wilaya ya Missenyi ina miradi miwili iliyopo Kata ya Kanyigo, pamoja na mpakani mwa Tanzania na Uganda, na kata ya kyaka bunazi.

Wilaya ya Karagwe ina miradi mitano iliyopo Kata Kayanga Omurshaka,ikiwa Biharamulo,Muleba,Ngara zinafanyiwa usanifu.

Amesema awali Mamlaka hiyo ilikuwa ikitoa huduma ya maji kwa wateja 14,046 waishio Manispaa ya Bukoba pekee.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,672FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles