BUJUMBURA, BURUNDI
SERIKALI ya Burundi imesema haitatoa ushirikiano kwa wachunguzi wa uhalifu wa kivita kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, ICC.
Vitendo vya uhalifu dhidi ya ubinadamu unadaiwa kufanywa na vikosi tiifu kwa Serikali ya Rais Pierre Nkurunziza dhidi ya wapinzani wa kisiasa.
Mahakama hiyo imeamuru uchunguzi rasmi juzi juu ya uhalifu uliotekelezwa kati ya Aprili 2015 hadi Oktoba 2017.
Hata hivyo, wataalamu wanasema itamuwia vigumu mwendesha mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda, kukusanya ushahidi pasipo kupata ushirikiano wa Serikali ya Burundi ambayo mwezi uliopita ilikuwa ya kwanza kujiondoa katika mahakama hiyo yenye makao yake makuu mjini The Heague nchini Uholanzi.