25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

WAATHIRIKA WA KIMBUNGA WASAIDIWA

HANOI, VIETNAM

NDEGE ya Urusi ambayo ina shehena ya tani 40 za mizigo ya misaada ya kibinadamu, imewasili nchini  Vietnam kuwasaidia waathirika wa kimbunga kilicholikumba taifa hilo hivi karibuni.

Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Misaada ya Mambo ya Dharura, ndege hiyo iliwasili juzi katika Uwanja wa Ndege mjini Cam Ranh, ikiwa ni baada ya Rais Putin kuiagiza Serikali yake kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha waathirika hao wanapata msaada.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa miongoni mwa shehena iliyomo ndani ya ndege hiyo ni mahema, vyakula, maziwa, makopo ya nyama na samaki.

Kimbunga hiyo aina ya Damri  kiliyakumba maeneo ya katikati mwa Vietnam mwishoni mwa wiki na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 60  na kujeruhi wengine kadhaa.

Mbali na kusababisha vifo na majeruhi, pia majengo yapatayo 80,000  yaliharibika na watu 40,000  wameokolewa huku baadhi ya maeneo katika nchi hiyo yamebaki bila umeme.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles