31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA MAREKEKIBISHO  YA SHERIA

 

Na ESTHER MBUSSI -DODOMA

BUNGE limepitisha muswada wa sheria tano zilizofanyiwa marekebisho zikiwamo Sheria za Mikataba ya Maliasili na Rasilimali za Nchi na Sheria ya Mahakama ya Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi.

Sheria nyingine ni   Upimaji wa Ardhi, Sura ya 324, Sheria ya Usajili wa Maofisa Mipango Miji, Sura ya 426 na Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, Sura ya 263.

Akiwasilisha bungeni muswada huo wa sheria mbalimbali, katika Sehemu ya Nne ambayo ni Sheria ya Mikataba ya Maliasili na Rasilimali za Nchi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alisema sheria hiyo ilivyo sasa haiko wazi kutamka kama madini na mafuta ni miongoni mwa maliasili na raslimali zilizoainishwa katika tafsiri ya maneno ‘natural wealth and resources’ iliyoko katika kifungu cha tatu cha sheria hiyo.

Katika marekebisho ya Sheria ya Mahakama ya Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi, Masaju alisema kifungu cha pili cha sheria hiyo kinatoa  tafsiri ya maneno, ‘Halmashauri ya Wilaya’ kuwa ni Halmashauri ya wilaya inayoanzishwa chini ya sheria ya Serikali za Mitaa sura ya 287.

Alisema  neno hilo limetumika kutambua vyombo vya utatuzi wa migogoro ya ardhi vinavyorejewa katika  sheria hiyo ikiwamo Baraza la Kata na Baraza la ardhi la Wilaya na kwa kuwa vyombo hivyo vinaweza kuanzishwa  katika maeneo mengine ya utawala ikiwamo miji, manispaa na majiji.

Katika  sheria ya Upimaji wa Ardhi,    Masaju alisema kifungu 4(3) cha sheria hiyo kinaweka masharti kuwa adhabu kwa mtu anayetiwa hatiani kwa kosa  la kufanya kazi za mpimaji chini ya kifungu hicho ni faini isiyozidi Sh 50,000 au kifungo cha miezi miwili  au vyote.

“Kifungu cha 6(2) cha sheria hiyo, kinaweka kuwa mtu anayetiwa hatiani kwa kosa la kupiga picha za anga kinyume na masharti ya kifungu hicho ni faini isiyozidi Sh 2,000, muswada huu unapendekeza adhabu kwa kosa hilo iwe faini isiyopungua Sh milioni tano au kifungo cha cha miaka miwili.

“Lengo ni kuweka adhabu inayoendana na wakati na kuwafanya watu kutenda kosa hilo kwani adhabu ya sasa ni ndogo na haimfanyi mtu kujirekebisha au kujutia kosa hilo,” alisema  Masaju.

Akitoa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF), alisema baada ya serikali kuamua kubomoa makazi ya wananchi hadi  eneo la  TAMCO Kibaha  mkoani Pwani, yamekuwapo   malalamiko ya wananchi.

Alisema wananchi hao wamedai Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), imebomoa nyumba zao wakati  lilikuwapo zuio la mahakama kubomoa nyumba hizo mpaka   maombi yao yatakaposikilizwa.

“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka serikali kueleza sababu za kubomolewa   baadhi ya nyumba  zilizokuwa na zuio la mahakama, au ieleze  kuhusu kauli ambazo zimetolewa na Rais kuwa wananchi wa  Mwanza hawatabomolewa kwa sababu walimpa kura.

“Tunapenda kujua kama huu ndiyo utaratibu mpya wa namna serikali inavyofanyakazi.

“Kama taifa hatutakiwi kuendekeza tabia kama hizi za kuingilia mifumo ya utoaji haki, ni vema masuala haya yakaheshimiwa na kufuatwa na kila  mtu kwa sababu hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria,

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles