29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Bunge kuwachunguza Trump na Saudi Arabia

NEW YORK, MAREKANI

WABUNGE wa chama cha Democrat katika Kamati ya Bunge kuhusu masuala ya ujasusi nchini Marekani wamesema watachunguza jinsi Rais Donald Trump alivyoshughulikia mauaji ya mwandishi wa habari wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi.

Kamati hiyo imesema mpango huo ni sehemu ya uchunguzi mpana kuhusu mahusiano kati ya Marekani na Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post toleo la jana, limesema kamati hiyo itachunguza tathmini ya Shirika la Ujasusi la Marekani, CIA, kuhusu mauaji ya mwandishi huyo, vita vya Yemen, uthabiti wa familia ya Kifalme ya Saudia na jinsi utawala huo unavyoshughulikia wakosoaji na waandishi wa habari.

Rais Trump, ambaye ana mahusiano ya karibu na utawala wa Saudi Arabia, amepuuza ripoti ya CIA kuwa mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia, Mohamed bin Salman, ndiye aliyeagiza Khashoggi kuuawa katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul nchini Uturuki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles