22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

BUKUNGU KURUDI KUICHEZEA MBEYA CITY

NA JESSCA NANGAWE

BEKI wa zamani wa Simba Mkongo, Besala Bukungu, yupo mbioni kurudi kuzichezea klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara na tayari ameanza mazungumzo na uongozi wa Mbeya City.

Bukungu, ambaye alimaliza mkataba msimu uliopita na klabu yake ya Simba, alirudi nchini kwao kuendelea na mambo mengine na sasa amesema atarejea wakati wowote kucheza Tanzania.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili, Bukungu alisema bado ana mapenzi makubwa ya kucheza soka la Tanzania na tayari ameanza mazungumzo na baadhi ya timu ili aweze kurudi kucheza.

“Bado nina mapenzi na klabu za Tanzania, napenda kuendelea kucheza, nashukuru nimeanza mazungumzo na baadhi ya klabu, ikiwamo Mbeya City, ambao wameonyesha nia ya kunihitaji, inawezekana wakati wowote nikamalizana na timu yoyote itakayoniridhia,” alisema Bukungu.

Katibu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, alisema wapo kwenye mchakato wa kuboresha kikosi hicho, lakini mpaka sasa hawajafahamu kama watamwongeza beki huyo.

“Tunafanya mchakato wa kuhakikisha tunapata kikosi kilicho bora, tutatumia dirisha hili la usajili kuongeza wachezaji wenye uwezo, siwezi kusema tumemalizana na Bukungu kwa sasa kwa kuwa mchakato bado unaendelea,” alisema Kimbe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles