27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Buhari aenda Uingereza kwa matibabu

Buhari_main_oneABUJA, NIGERIA

RAIS wa Nigeria, Muhammadu Buhari ameanza likizo ya siku 10 jana ambayo itamkuta mjini London, Uingereza kwa matibabu zaidi.

Mshauri Maalumu wa Rais wa Vyombo vya Habari na Uenezi, Femi Adesina, alisema kiongozi huyo wa Nigeria jana alitarajia kuelekea London kwa likizo na kutumia fursa hiyo kuonana na daktari kutokana na kuzidi kwa uambukizo sikioni.

Kwa mujibu wa Adesina, Rais Buhari awali alifanyiwa uchunguzi na daktari wake binafsi pamoja na mtaalamu mwingine mjini Abuja, na kutibiwa.

“Madaktari wote hawa wawili wa Nigeria walishauri uwepo uchunguzi zaidi ng’ambo, kama tahadhari zaidi,’’ alisema katika taarifa yake.

Rais Buhari alisitisha ratiba zake za kikazi kipindi cha wiki chache zilizopita, ikiwamo kufuta ziara dakika za mwisho katika eneo lenye machafuko na tajiri kwa mafuta la Niger Delta.

Mwezi uliopita mtawala huyo wa zamani wa kijeshi mwenye umri wa miaka 73 alifuta kile kilichotarajia kuwa ziara yake ya kwanza tangu aingie madarakani katika jiji kuu la kibiashara – Lagos.

Pia alishindwa kuhudhuria uzinduzi wa mradi wenye thamani ya dola bilioni moja wa usafishaji eneo tajiri la mafuta la Ogoniland.

Buhari aliingia madarakani Mei 2015 baada ya kushinda uchaguzi kutokana na ahadi yake ya kupambana na ufisadi pamoja na wanamgambo wa Kiislamu wa Boko Haram.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles