26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

BRELA yawanoa Wahariri kuhusu maboresho ya kisheria

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari nchini wamepewa elimu ya marekebisho na maboresho ya kisheria na kimfumo wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), kwenye utekelezaji wa kanuni za wanufaika wa mwisho katika kampuni lengo likiwa kuboresha huduma zinazotolewa na Wakala ili wapate nafuu na urahisi wa kufanya biashara nchini.

Akizungumza leo Juni 8, jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo ya uhamasishaji wa utekelezaji wa kanuni za wanufaika wa mwisho katika kampuni(Beneficial Owners) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu Brela, Mkurugenzi wa Leseni, Andrew Mkapa amesema wahariri ni wadau muhimu kwasababu ndiyo nyenzo muhimu inayotegemewa katika kufikisha taarifa mbalimbali kwa jamii.

“Kutokana na hali hiyo Brela inatambua nafasi ya wahariri kuwa ni kiungo muhimu na chachu katika Nyanja ya uhamasishaji urasimishaji biashara nchini,”amesema Mkapa.

Amesema Brela imekuwa ikiwashirikisha wanahabari hususan wahariri kwenye shughuli zake mbalimbali zinazohusu utendaji kazi wa kila siku pamoja na marekebisho na maboresho mbalimbali ya kisheria na kimfumo.

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri(TEF), Deodatus Balile amesema Brela wamezingatia umuhimu wa kundi hilo kama wadau wakubwa.

“Brela imekuwa ikishirikiana na wanahabari hususan wahariri kwenye shughuli zake mbalimbali zinazohusu utendaji kazi wa kila siku na pale tunapokuwa na jambo jipya na la kimkakati.

“Hii ni pamoja na kupeana taarifa kunapotokea marekebisho na maboresho mbalimbali yanayoendelea ya kisheria na kimfumo ili kuhakikisha kuwa tunakuwa na uelewa wa kutosha kwenye habari tunazozipeleka kwa wananchi kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara nchini,” amesema Balile.

Amesema warsha hiyo imetoa ufafanuzi zaidi wa maboresho yanayoendelea kwenye sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya ya huduma za usajili wa Kampuni hususan mabadiliko ya 2022 na kanuni zake.

“Niwakumbushe tu kwamba, Bunge lilipitisha marekebisho ya Sheria ya Kampuni, Sura ya 212 kwa lengo la kuwezesha upatikanaji wa taarifa za Wamiliki Manufaa katika kampuni zote ambazo zilikwisha sajiliwa na zinazoendelea kusajiliwa ili kuboresha mazingira ya uwekezaji, kuzuia ukwepaji kikodi pamoja na kudhibiti utakatishaji fedha haramu na ufadhili wa vitendo vya ugaidi,” ameongeza Balile.

Aidha, Balile amesema kuwa Brela imeshaanza utekelezaji wa ukusanyaji na utunzaji wa taarifa za Wamiliki Manufaa wa Kampuni.

“Takwimu zinaonesha kwamba, Kampuni nyingi bado hazijawasilisha taarifa hizo, hivyo basi, kwa kuzingatia umuhimu wenu kama njia muhimu ya kuwafikishia Umma taarifa, Brela wameandaa Warsha hii mahususi kwa ajili ya kupeana uzoefu na uelewa wa pamoja ili kuifikishia jamii taarifa sahihi,”amesema.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kupitia vyombo vya Habari itasaidia Watanzania kuwakumbusha juu ya muda, taratibu na umuhimu wa uwasilishaji wa taarifa za Umiliki manufaa katika kampuni mujibu wa sheria.

Naye Mkuu wa Sehemu ya Usajili wa Makampuni (Brela), Isdor Nkindi amesema miongoni mwa majukumu ya Brela ni usajili wa kampuni, majina ya biashara, alama za biashara na huduma, kutoa hataza, leseni daraja la kwanza pamoja na kutoa leseni za viwanda.

Amesema warsha hiyo imekuwa ya kuhamasisha dhana ya umiliki manufaa (Beneficials owner) pamoja na kuhamasisha kuwasilisha taarifa za kila mwaka(Annual Returns) ambazo ni takwa la kisheria kwa kila kampuni au jina la biassara kuwasilsiha taarifa zake.

Amesema mfanyabiashara asipowasilisha hizo taarifa adhabu ipo kisheria ikiwemo kufutwa kwa jina la biashara hio iliyompa msajili kudhani biashara hiyo haipo tena.

“Sisi si lengo letu kufuta hizo biashara tunahamasisha kutekeleza takwa hilo la kisheria la annual returns,”amesema.

Amesema mwaka 2018, Brela ilianza kutoa huduma zote kwenye mfumo wa kielekroniki ambapo kampuni ambazo zilisajiliwa nyuma yam waka 2018 zipo kwenye karatasi hivyo wanahuisha ili ziende kwenye mfumo wa kidigitali.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kampuni na Majina ya Biashara, Meinrad Rweyemamu amesema kuwa Brela na vyombo vya Habari vimekuwa na ushirikiano katika kutoa elimu na kuelimisha umma kazi zinazofanywa na Brela.

Amesema sheria inaeleza taarifa za wamiliki kampuni zinatolewa kwa vyombo vya uchunguzi ambapo inapaswa iwepo taarifa ambapo kila kampuni inapaswa kutoa taarifa zake kwa msajili wa kampuni za walimiki manufaa.

“Dhana ya wamiliki manufaa ni kw amba kuna watu wanaingia kwenye kampnuni lakini hawataki kuonekana, huku awali hatukuwa na idadi hivyo tulipaswa kuwa na orodha ya wamiliki manufaa inayoonesha wamiliki kampuni, mnufaika, mtoa maelekezo, mtoa fedha,”mesema Rweyemamu.

Mmoja wa wahariri walioshiriki warsha hiyo, Jenifer Sumi amesema mafunzo hayo yatawasaidia kupata ufahamu wa kina kuhusu usajili wa kampuni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles