25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Jamii bado inahitaji elimu kuhusu uchangiaji damu

Na Safina Sarwatt, Moshi

Kituo cha Damu Salama Kanda ya Kaskazini kinatarajia kukusanya chupa 875 katika kampeni ya changia damu ambapo kwa siku zitakusanywa chupa 60.

Akizugumza na Waandishi wa Habari mkoani Kilimanjaro Juni 7, 2023 Afisa Uhamadishaji Kanda ya Kaskazini, Feisal Abubakar amesema bado uhitaji wa damu ni mkubwa.

Mashine ya kuchakata mazao ya damu.

Aboubakar amesema kampeni hiyo ya uchagiaji wa damu inafanyika katika maeneo mbalimbali ikiwemo vyuo, kanisani, msikitini na vituo vya mabasi lengo likiwa ni kuhakikisha wanafikia malengo.

Amesema kampeni hiyo imeshirikisha wadau mbalimbali kambi za jeshi, red cross na vilabu vya uchangiaji damu shuleni na vyuoni.

Amesme kuwa wapo baadhi ya watu wamekuwa na imani potofu kwamba wakichangia damu wanawepoteza maisha yao ama kupatwa na madhara ya kupungukiwa damu jambo ambalo siyo kweli.

“Elimu bado inahitajika zaidi kuhusu uchangiaji damu kutokana na baadhi ya watu kuwa na imani potovu kwamba wakichangia damu wanawepoteza maisha au watapatwa na matatizo huku wengine wanahofia kupimwa VVU kwa nguvu,” amesema Aboubakar.

Katika hatua nyingine ametoa wito kwa jamii kujitokeza kuchangia damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya watu huku akisisitiza kwamba damu haiuzwi ni bure.

“Mtu yoyote asijaribu kumshawishi mhudumu wa afya kumpa fedha ili apate huduma ya kuongezewa damu kufanya hivyo ni kosa damu ni bure,”amesema.

Amesema kuwa asilimia kubwa wachangiaji wa damu ni vijana hivyo ametoa rai kuendelea kujitokeza kushiriki mara kwa mara kuchangia damu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles