33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Brela yakunwa mwamko uombaji leseni njia ya mtandao

Na Clara Matimo, Mwanza

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela),imeeleza  kuwa kwa sasa kuna mwitikio mkubwa wa wananchi kusajili biashara zao na kuomba leseni baada ya mapinduzi  ya uombaji huo kwa njia ya mtandao.

Hayo yameelezwa na Ofisa Usajili Kitengo cha Kampuni  Majina ya Biashara wa Brela, Angela Kimario, alipozungumza na MTANZANIA Digital iliyotembelea banda lao lililopo viwanja vya Rock City Mall jijini hapa kwenye maonesho yanayoendelea ya biashara ya Afrika Mashariki.

Amesema maombi ni mengi ikilinganishwa na walipokuwa wanapeleka maombi ofisini hivyo mfumo huo umesaidia kuwafikia karibu zaidi wananchi na unawawezesha  kupata huduma saa 24.

“Ili uweze kusajiliwa Brela unahitaji vitu vichache sana ambavyo ni namba ya nida, barua pepe na namba ya simu  hivyo nawasihi sana wananchi wasajili biashara zao naamini uwezekano wa kupata vitu hivyo vitatu nilivyovitaja upo,”amesema Kimario.

Amesema Brela inasajili majina ya biashara, kampuni,  wanatoa leseni za viwanda biashara kundi A ambayo inamruhusu mfanyabiashara kufanya biashara popote nchini na nje ya nchi, hataza na alama za biashara.

“Lakini kila penye mafanikio hapakosi changamoto, hivyo na sisi pamoja na mwitikio mkubwa wa wananchi kusajili biashara zao kwa njia ya mtandao, changamoto inayotukabili ni baadhi ya wananchi wanashindwa kutumia mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao lakini wale wanaokuja kwenye banda letu hapa wanapata fursa nzuri ya kujifunza maana tunawafundisha na kuwasajilia wanaondoka  na vyeti vyao.

“Unaposajili  unakuwa umeirasimisha biashara yako  inajulikana kisheria na inakupa utu wa kisheria, hivyo wafanyabiashara watambue kwamba ni muhimu sana kusajili kampuni au jina la biashara maana unapata fursa mbalimbali mfano mikopo kutoka taasisi za fedha pia unaweza kupata zabuni mbalimbali,”ameeleza Kimario.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Brela, Roida  Andusamile, amesema mara kwa mara hushiriki maonesho hayo lengo ni kuwapatia   elimu wadau wanaotembelea banda lao kuhusu huduma wanazozitoa 

ambao wengi wao huvutiwa na faida za kusajili biashara zao hivyo huwasajili na kuwapa vyeti vyao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles