23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Brazil yamtangaza Tite kuwa kocha mpya

Adenor Bacchi ‘Tite’
Adenor Bacchi ‘Tite’

RIO DE JANEIRO, BRAZIL

SHIRIKISHO la Soka nchini Brazil (CBF), limemtangaza kocha mpya wa timu hiyo, Adenor Bacchi ‘Tite’ ambaye anachukua nafasi ya Carlos Dunga.

Dunga amefukuzwa kwa mara ya pili baada ya timu hiyo kutolewa katika hatua ya makundi kwenye michuano ya Kombe la Copa America ambayo inaendelea kutimua vumbi nchini Marekani.

Katika michuano hiyo, mchezo wa kwanza Brazil ilitoka sare ya bila kufungana dhidi ya Ecuador, wakati mchezo wa pili Brazil ilishinda mabao 7-1 dhidi ya Haiti huku mchezo wa mwisho wakikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Peru na kusababisha kocha huyo kufukuzwa.

CBF imesema wamemfukuza Dunga kutokana na kushindwa kufanya vizuri katika michuano ya Copa America kwa misimu miwili mfululizo pamoja na kuanza vibaya katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia.

Kocha mpya Tite, awali alikuwa anaifundisha klabu ya Sport Club Corinthians Paulista, ambayo inashiriki ligi nchini Brazil na alishinda mataji mawili akiwa na timu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles