29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Brazil wawajibu mashabiki zao

SAO PAULO, BRAZIL

TIMU ya taifa ya Brazil, imewajibu mashabiki zao ambao walikuwa wanaizomea timu hiyo baada ya kulazimishwa suluhu dhidi ya Venezuela kwenye michuano ya Copa America.

Brazil ni wenyeji wa michuano hiyo, katika hatua ya makundi mchezo wao wa kwanza walifanikiwa kushinda mabao 3-0 dhidi ya Bolivia, lakini mchezo wa pili Brazil wakatoka suluhu kabla ya mchezo wa usiku wa kuamkia jana kushinda mabao 5-0 dhidi ya Peru.

Ushindi huo wa jana unadiwa ulitokana na kiwango cha hali ya juu ambacho kilioneshwa na Brazil, hivyo wameweza kuwajibu mashabiki wao, hivyo Brazil wamefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali kutokana na mabao yaliyowekwa wavuni na Casemiro, Roberto Firmino, Everton, Dani Alves na Willian.

“Huu ulikuwa moja kati ya mchezo wetu bora, hii inatokana na ubora wa uwanja, tunaamini kama eneo la kuchezea lipo vizuri basi lazima tuonesha kiwango cha hali ya juu, tunaweza kusema tulikuwa na wastani wa pasi 600 tulizopita,” alisema kocha huyo.

Hata hivyo, aliongeza kwa kusema, lazima wahakikishe wanapambana na wanaendelea na kiwango hicho kwenye ardhi ya nyumbani ili kuweza kuchukua taji hilo la bara la America.

“Kama tutaendelea kucheza kwenye kiwango hiki, basi tuna nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa, nimewaambia wachezaji kwamba, lazima wawe tayari kwa ajili ya kucheza kwenye hali yoyote.

“Tumecheza katika aina ya soka letu, hii inaweza kutufanya tukajiamini mbele ya mashabiki zetu, vizuri kupambana kwa ajili ya taifa na pia kutowaangusha mashabiki kwenye ardhi ya nyumbani,” aliongeza kocha huyo.

Brazil wanashiriki michuano hiyo bila ya uwepo wa mshambuliaji wao hatari Neymar JR ambaye anasumbuliwa na enka baada ya kuchanika kwenye moja ya mchezo wa maandalizi ya michuano hiyo, hivyo mchezaji huyo ambaye anakipiga katika klabu ya PSG atakuwa nje ya michuano hiyo hadi mwisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles