30.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Sane awatoa wasiwasi Manchester City

MANCHESTER, ENGLAND

MSHAMBULIAJI wa pembeni wa mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City, Leroy Sane, amewatoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo kuwa hana mpango wa kuondoka na yupo tayari kuzungumza na uongozi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, alikuwa anahusishwa kutaka kutua katika kikosi cha mabingwa wa soka nchini Ujerumani, Bayern Munich, lakini amefanya mazungumzo na rafiki zake wa karibu na kuwaambia hawezi kuondoka Man City kwa sasa.

Awali mchezaji huyo aligoma kuongeza mkataba mpya akishinikiza kutaka kuondoka kutokana na kukosa nafasi ya kudumu. Msimu uliomalizika amecheza jumla ya michezo 47 na kufunga mabao 16 huku akitoa pasi 18 za mwisho.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun nchini Uingereza, mchezaji huyo amebakisha miaka miwili kumalizana na Manchester City, lakini amesema yupo tayari kuongeza mkataba mpya.

Sane alijiunga na Manchester City mwaka 2016, akisaini mkataba wa miaka mitano wa kuutumikia uwanja wa Etihad. 

Mchezaji huyo amekuwa akikosa namba ya kudumu kwenye kikosi hicho kutokana na uwepo wa Raheem Sterling pamona na Bernado Silver ambao walikuwa bora msimu uliomalizika katika safu ya ushambuliaji wa pembeni.

Hata hivyo mchezaji huyo amedai atahakikisha anajiandaa kwa ajili ya kupigania namba kwenye kikosi cha kwanza kwa ajili ya kitimiza ndoto zake.

Moja ya sababu ambayo mchezaji huyo inatajwa ilimfanya ashuke kiwango ni kutokana na kuachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa Ujerumani kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi, ikiwa kabla ya kuitwa kwa kikosi hicho alikuwa ametajwa kuwa mchezaji bora chipukizi nchini England kwa msimu wa mwaka 2017/2018.

Miongoni mwa klabu zingine ambazo zilianza kuonesha nia ya kumtaka mchezaji huyo ni pamoja na Manchester United, lakini waliamua kujitoa mapema kwenye mbio hizio za kuwania saini yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles