WASHINGTON, MAREKANI
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF), Christine Lagarde amezitaka Marekani na China kusuluhisha mvutano wao wa kibiashara kupitia msingi wa kanuni za taasisi za pande nyingi.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa Kamati ya Kutunga Sera ya IMF, Lagarde amesema Marekani na China zinapaswa kufanya kazi kwa msingi wa biashara huria na ndani ya mfumo wa msingi wa taasisi za pande nyingi.
Ushauri wa Lagarde umekuja wakati Waziri wa Fedha wa Marekani, Steven Mnuchin akisema anafikiria kufanya ziara nchini China ili kujadili masuala ya kibiashara na wenzake wa China.